Mwanadada mtangazaji Diva aka the Bawse, yupo tayari kubadili dini ili aweze kuolewa na mwanaume aitwaye Omar Borkan, na wala mtangazaji huyo hatojali hata akiwa mke wa ngapi, ilimradi aolewe na mwanaume huyo. Kupitia mtandao wa instagram mtangazaji huyo alipost picha ya mwanaume huyo na kuandika manano haya ” Hata dini ntabadili wallah… Anioe tu huyu kaka … Hata mke wa ngapi poa @omarborkan isn’t he just a cute man on earth guys? ”
Omar Borkan ni mwanaume mwenye asili ya kiarabu na anafanya shughuli za Photographining, mwandishi wa mashahiri na pia ni Actor kutoka Dubai, mwanaume huyu anamvuto kiasi cha kuwachanganya wakina dada wengi.
Kutokana na mvuto wake huo, Omar Borkan alishawahi kuponzwa na umvuto wake alionao kiasi cha kufikia kufukuzwa katika moja ya sherehe Riyadh na polisi wa kidini ya kiislam. Na pia kaka huyu alipewa amri ya kuondoka kabisa nchini Saudi Arabia kwa kuwa atakuwa akiwachanganya wanawake kwa mvuto wake.
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII