BREAKING NEWS: ZITTO KABWE NA DR KITILA MKUMBO WAVULIWA VYEO VYAO VYOTE CHADEMA
Kikao cha Kamati Kuu ndiyo kimeisha muda huu, na taarifa zilizopo ni
kwamba kambi ya PM7 imevunjwa rasmi baada ya viongozi wake kuvuliwa vyeo
vyote walivyo navyo ndani ya chama.
Waliovuliwa vyeo ni Zitto Kabwe, ambaye amevuliwa nafasi ya Naibu Katibu
Mkuu wa chama pamoja na nafasi ya Naibu wa Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni. Dr. Kitila Mkumbo yeye amevuliwa nafasi ya mjumbe wa kamati
kuu.
Kamati Kuu imewaandikia barua Zitto na Kitila, wajieleze ndani ya siku 14 kwanini wasifukuzwe uanachama.
CHANZO: JAMII FORUM
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII