Pages

Thursday, November 14, 2013

HIZI NDIZO PICHA ZA SHEHENA YA PEMBE ZA NDOVU ZILIZOKAMATWA ZANZIBAR


Kamanda wa Kikosi cha Polisi Bandarini Zanzibar akiongoza Operesheni wa kukagua magunia yaliyokuwa na Pembe za Ndovu yaliokamatwa katika bandari hiyo leo yakiwa katika harakati ya kusafirishwa nje ya nchi kupitia bandari hiyo, zoezi hilo limefanywa chini ya Jeshi la Polisi Bandari Kikosi cha KMKM, yalikuwa katika Kontena la futi 40.
Magunia haya yakiwa na shehena na makombe ya Pwani wakati katikati yakiwa na viroba vya Pembe za Ndovu ambazo zilikuwa zimehifadhiwa katika Kontena likiwa tayari kusafirishwa nje ya Nchi, limegunduliwa katika bandari ya Zanzibar leo asubuhi.
Baadhi ya Pembe za Ndovu zilizokamatwa katika bandari ya Malindi Zanzibar yakisubiri kuhesabiwa kupata idadi kamili, thamani yake na uzito kwa ujumla.
Operesheni ya kuhesabu Pembe za Ndovu zilizokamatwa katika bandari ya Zanzibar ikiendelea.
(Picha kwa hisani ya Michuzi Blog)

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII