TUHUMA nzito zinamkabili rapa wa Bendi ya Akudo
Impact ‘Wazee wa Masauti’, Kanal Top (pichani) ambaye anadaiwa kunaswa
na madawa ya kulevya ‘unga’ nchini China, Risasi Jumamosi
limenyetishiwa.
Rapa wa Bendi ya Akudo Impact ‘Wazee wa Masauti’, Kanal Top (pichani).
Meneja wa Bendi ya Akudo Impact, Ramadhan Pesambili, Novemba 14, mwaka huu ameliambia Risasi Jumamosi kwamba wamepata taarifa za kushikiliwa kwa Kanal Top nchini China kwa tuhuma hizo.
“Taarifa hizo tumezisikia, tunazifuatialia kwa umakini mkubwa na kuweza kujua kama ni kweli ama la, maana zinachanganya sana,” alisema Pesambili.
Aidha, meneja huyo ameonesha kusikitishwa na habari hizo na kudai kwamba zinaichafua bendi yao kutokana na watu mbalimbali kumpigia simu kumuulizia juu ya taarifa hizo na wengine kumfafanulia zaidi jinsi Kanal Top alivyonaswa.
“Kama meneja wa Akudo nasikitishwa na taarifa hizo, kwa kuwa Kanal Top hatuko naye zaidi ya miezi minne sasa, mwanzo aliaga anakwenda Kongo kuoa na aliporudi aliomba ruhusa ya kwenda Dubai kufanya shoo ya wimbo wake wa Mama Vanesa nasi tukamruhusu kwa moyo wote.
“Wiki tatu zilizopita tulisikia habari za uvumi huo na tulipofuatilia tukagundua si kweli,” alisema meneja huyo.
Pesambili alisema kuwa hata Mzee Kapuya (Juma, mmiliki wa Akudo) alisikia uvumi huo na akasema kama kweli Kanal Top anajihusisha na biashara hiyo basi asirudi kwenye bendi yake na ikiwezekana akamatwe kabla hajachafua hali ya hewa.
“Lakini kabla hatujachukua hatua zozote ndiyo juzi tukasikia tena kuwa amekamatwa nchini China.
“Viongozi wa Akudo tumesikitishwa sana na taarifa hizo ingawa bado tunaendelea kuzifuatilia ili tuweze kujua zaidi, maana tunasikia amekamatwa akiwa na wanamuziki wa FM Academia, wengine wanasema alikuwa na mkewe,” alisema Pesambili huku akikiri simu ya China ya Kanal Top haipatikani.
SOURCE : GPL

No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII