USHAHIDI WA NYARAKA ZA MALIPO ZINAZOMHUSU ZITTO KABWE NDIO HUU HAPA

Na Yericko Nyerere.

Jamiiforums

Baada ya Mh Lema kumtuhumu Mh Zitto kuwa ni MNAFIKI kwenye suala la POSHO na hana uzalendo wowote,

Mh Zitto Kabwe alijibu hivi:



Quote By Zitto
Habari/tuhuma hizi sio za kweli. PAC ni marufuku kupokea posho kutoka Taasisi au Mashirika. Ni marufuku kabisa. Namtaka Lema, atoe ushahidi kuwa kamati ya PAC wajumbe wake wanalipwa posho yeyote ile.

Toka nimekuwa mwenyekiti wa POAC sio tu nilipiga marufuku posho bali pia niliwashitaki PCCB wabunge wanaochukua posho kutoka kwa taasisi za Serikali. Wabunge walihojiwa na PCCB kuhusu jambo hili mpaka Sitta alipoingilia kati kuwatetea. Hiyo ilikuwa mwaka 2009 kabla yeye (Lema) hajawa mbunge.-

Wabunge wajumbe wa kamati ya PAC wanalipwa posho za vikao kama wabunge wengine lakini mimi sichukui posho hizo za vikao.

Sio tu PAC hata kwenye Baraza la madiwani na Baraza la Mashauriano la mkoa wa Kigoma na popote kule. Hata NGO zikinialika kwenye vikao vyao sichukui posho za vikao. Nafasi yoyote ninayoalikwa kama mbunge sichukui posho za vikao.-

Yeyote mwenye ushahidi wa mimi kuchukua posho za vikao popote pale auweke hadharani na nitawajibikaSio kuandika uzushi au maneno ambayo mtu yeyote anaweza kuandika.-

Mimi siwezi kubishana na Lema maana ni kiongozi wake katika chama. Natumaini kadiri anavyokaa kwenye uwanja huu wa siasa atabadilika na kukomaa zaidi.

HAPA CHINI SASA NI USHAHIDI DHI YAKE
Tunaanza na hii nyaraka zingine zitafuaata:

Kwakuwa Zitto aliomba kuwekwa ushahidi wa kinyaraka ili kukidhi madai/tuhuma za Mh Lema kwake


Maswali:

1. Zitto Z. Kabwe, katika utetezi wako ulisema kuwa huwa hupokei posho wala marupurupu kutoka kwenye taasisi yoyote ya umma inayoratibiwa na kamati yako ya POAC, Sasa waeleze watanzania kuwa ni taasisi gani iliyokugharimia ulipokuwa MOUNT MERU HOTEL tangu tarehe 30/08/2013 hadi 05/09/2013 na ukatumia shilingi 1,148,000 ilihali mshahara wako hauzidi milioni mbili kwa mwezi?


UFAFANUZI:

Kwanini invoice haijasainiwa na Zitto?


a) Kwa wale mnaojua maana ya hotel za kisasa au biashara za kisasa nikuwa risiti huwa kwenye data base ya hotel husika, hivyo mteja huprintiwa risIti yake na kuisaini yake tu na kuondoka nayo ikiwa ni pamoja na risiti ya TRA, 

Hotel husika hubaki na kopi iliyopo kwenye data base ya hotel hiyo,

na hii ndio kopi HALALI ya GHARAMA alizotumia huyu MZALENDO wa MDOMONI tu lakini matendo yake ni fisadi,

b) Wale wanaohoji kuwa mbona invoice ni ya 4/11/2013?

watambue kuwa leo ndio imetolewa kwenye data base ya hotel husika hivyo data base lazima itarekodi tarehe ya leo,

muhimu watu waangalie siku alipoingia na kutoka


UPDATES

Kutoka kwa Nassar 



Quote By Joshua Nassar
Tarehe 16 sept 2013 alisafiri kwenda malaysia kama mkiti wa PAC na wabunge wengine toka kamati nyingine. Akalipwa posho kwa siku 10 posho ameshalipiwa na nssf hotel, transport na meals zote alafu akalipwa dola 750 kwa siku zote( kosa).

2. Akiwa malaysia akapiga dili nyingine akadandia ziara ya NHC ambao walikuwa singapore kwa ajili ya mradi wao wa tanganyika packers kawe. Najua walikuwepo wabunge wa kamati husika, alikuwepo mbunge wa kawe pia, jamaa naye akairukia tar 19 sept akawatoroka wabunge wenzake malaysia akaenda singapore. Uko nako akalipwa tena posho then akarudi dubai tar 22 kuungana na wale aliowaacha malaysia. (Double payment)

Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network
=====================


UPDATES,

Hapa chini ni NYARAKA za SLEEPING Allowance na POSHO ambazo TANAPA na WIZARA ya MAMBO YA NDANI wamemlipia ZITTO,


Attached Files

Invoice For Accomodatiion.pdf



UPDATES ZA LEO 6/11/2013
Hapa chini ni NYARAKA za Mamilioni ya POSHO/Allowances yalivyo tafunwa na POAC ya Zitto,

NB

Katika nyaraka hizi kunaufisadi mkubwa uliofanya na Zitto Kabwe, Pius Msekwa na Shams Mwangunga,

Zisomeni kwa umakini.

HII HAPA NI Nyaraka ya malipo ya SITTING ALLOWANCE

Click image for larger version. 

Name: 20131106_110146.jpg 
Views: 0 
Size: 2.66 MB 
ID: 120020





Hapa jioneeni wenyewe ufisadi wa Zitto anaedai ni mzalendo, Hapa walilipiwa ndege kwa gharama ya zaidi ya MILIONI MIAMOJAKUTOKA DAR KWENDA ARUSHA, PIA WAKALIPANA POSHA ZAIDI YA MAMILIONI,



SWALI,

Zitto Zuber Kabwe ni mzalendo na anahaki ya kuwatumikia Watanzania kwakujinasibisha na uzalendo uliotukuka katka ardhi ya Tanzania?


Nyaraka zingine zinakuja,

hapa ninashehena ya nyaraka zake zakutosha kabisa,



UPDATES 7/11/2013

Kabla ya kuwapa video, nawapa nyaraka hii,

Hapa alisafiri kwenda nchini Rwanda kwa siku TATU, lakini akalipwa posho ya SIKU KUMI,

Huyo ndie MZALENDO ndugu Zitto Kabwe,


Ufafanuzi juu ya kuchukua posho ya sku kumi na kufanya kazi kwa siku tatu,
Izingatiwe kuwa SAFARI ya Rwanda ilikuwa ya siku kumi kutoka tarehe 10/6/211 kwa mjibu wa nyaraka za kibunge,
Lakini tarehe 15/6/2011 Zitto Kabwe alikuwa Bungeni akisimo hotuba ya kambi rasmi ya upinzani, ushahidi upo, na tarehe 16/6/ alichangia bungeni, ushahi wa hansadi za bunge upo, hivyo nyaraka zilizopo zinamuuonyesha Mh Zitto alisafiri kwenda Rwanda kwa siku tatu tu, ushahidi upo,

Click image for larger version. 

Name: image 20.jpg 
Views: 0 
Size: 1.52 MB 
ID: 120174
Attached Thumbnails Attached ThumbnailsClick image for larger version. 

Name: 20131106_110209.jpg 
Views: 0 
Size: 3.01 MB 
ID: 120021  
 Attached Images

 Attached Files
Chanzo cha Habari hii ni jamiiforums
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs