Pages

Wednesday, December 18, 2013

KWELI BONGO HAMNA SIRI, WEMA TAABANI....ADAIWA KUFULIA VIBAYA

Wema Isaac Sepetu.
Stori: Oscar Ndauka na Richard Manyota
NI kweli hakuna marefu yasiyokuwa na ncha? Kama ni kweli, basi ile jeuri ya fedha ya Miss Tanzania mwaka 2006 ambaye pia hufanya vyema kwenye gemu la sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu inadaiwa imefikia nchani, Risasi Mchanganyiko limepashwa ‘ei tu zedi’.

Baadhi ya magari anayomiliki Wema.
Kwa mujibu wa chanzo makini, hali ya kifedha ya staa huyo si nzuri kiasi kwamba kwa sasa amekuwa mtu wa kushinda ndani kwa kuwa hana mpunga unaomuwezesha kwenda kujirusha kama zamani.

SABABU NI NINI HASA?
Chanzo kilidai kwamba, binadamu aliyekuwa akimmwagia manoti staa huyo aliyetajwa kwa jina moja la Clement ambaye ni mwajiriwa wa Ikulu jijini Dar, yu hoi kwa kipato baada ya kunyofolewa kwenye kitengo kilichokuwa na uwezeshaji mwingi wa fedha.
Wema akiwa ofisini kwake.
Inadaiwa kuwa, baada ya Clement ambaye ni mume wa mtu, kuondolewa kwenye kitengo hicho amepelekwa sehemu nyingine ambayo mchana kutwa ni kupiga miayo mpaka muda wa kutoka kazini.

MKONO WA MKEWE WATAJWA
Katika madai hayo, inasemekana mke wa Clement (jina tunalo) ana mkono wa kile kilichompata mumewe, kuondolewa kwenye kitengo chenye ulaji na pia amekuwa akiwawinda wawili hao ili awafanyie fumanizi kwa sababu Clement ni mumewe wa ndoa.
Wema akiwa ndani ya nyumba aliyodai yake.
KILICHOTOKEA SASA
Chanzo kikaendelea: “Baada ya kuondolewa kwenye sehemu yenye fedha na kutupwa kwenye ukame, jamaa akaanza kupata tabu kwani fedha alizokuwa akimpa Wema zamani zikawa hazipo.
“Hilo likamwathiri na Wema mwenyewe kwani ile jeuri mliyokuwa mnamuona nayo akiifanya kwa rungu la fedha, mara sherehe, mara kumlipia Kajala (Masanja) makahamani (Kisutu), mara kwenda baa na wapambe imekatika ghafla.
“Siku hizi Wema ndani na yeye, yeye na ndani. Naamini hata mkienda kwake muda huu (juzi Jumatatu saa 5 asubuhi) mtamkuta.”

INADAIWA AMEUZA MAGARI MAWILI
Habari zaidi kutoka chanzo hicho, hali ilipozidi kubana sana, Wema aliamua kuuza magari mawili kati ya matatu anayomiliki ili apate fedha za kuendelea kujikimu katika maisha ya kila siku.
Magari hayo mawili yanasemekana ni Toyota Mark II GX 110 na Toyota Harrier na kubakiwa na Audi Q7.

YALIYOMPATA CLEMENT
Habari zinazidi kudai kwamba hali ikazidi kuwa mbaya kwa Clement kiasi kwamba alijikuta akikabwa koo na benki moja ya jijini Dar es Salaam ambayo aliiomba mkopo wa Shilingi mil. 120 akitumia hati ya nyumba ambayo pia si yake.
Benki hiyo ilipozidi kumbana, mkewe (sasa wametengana) ambaye naye anadaiwa kuwa ‘mzuri’ kwenye fedha alikwenda kulipa fedha hizo benki ili nyumba ya watu isinadiwe na benki hiyo iliyokuwa haitaki mambo ya utani kwenye marejesho.
Madai mengine ambayo hayajathibitishwa yanasema kuwa, mtikisiko huo wa kifedha kwa Clement umesababisha awe ‘choka mbaya’ kiasi cha sasa kuanza kupiga mizinga kwa rafiki zake.

WEMA ASAKWA ASEME UKWELI WAKE
Baada ya kupokea ishu hiyo, Risasi Mchanganyiko liliamua kumsaka Wema ili aseme lolote kuhusiana na tuhuma hizo.
Saa 4:32 Wema alipigiwa simu yake ya mkononi ambayo iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa hata pale iliporudiwa tena na tena.
Baada ya jitihada hizo kugonga mwamba, gazeti hili liliamua kumwendea hewani meneja wake Martin Kadinda ambaye naye hakupokea simu licha ya kupigiwa zaidi ya mara tatu.
Risasi Mchanganyiko halikukata tamaa, kwani ni haki ya msingi kwa Wema kuongelea suala hilo. Likampigia msaidizi wake wa karibu anayeitwa Pat Man, yeye alipokea, akaulizwa kuhusu bosi wake huyo, akasema:
“Wema anaumwa (hakutaja ugonjwa), ametoka hospitali sasa hivi  (hakusema hospitali gani) yuko nyumbani.”
Mapaparazi wetu wakafunga safari kutoka Bamaga – Mwenge, Dar yalipo Makao Makuu ya Nyumba ya Magazeti Pendwa Bongo, Global Publishers hadi nyumbani kwa Wema - Makumbusho (lakini ni Kijitonyama).
Getini alikutwa mlinzi mahiri kwa mwonekano ambapo alipoombwa kumwita Wema au kumwambia kuna waandishi wa Global wapo nje, alisema:
“Mh! Kwa kweli si rahisi kutoka, amelala anaumwa... alikwenda hospitali amerudi muda si mrefu.”
Alipochombezwa kwa maneno ya ‘kisiasa’ kwamba awaambie wasaidizi wake wa ndani wakamwamshe, alikataa akisema litazuka timbwili ambalo yeye hakuwa tayari kuliona.
“Bosi akilala huwa hapendi kuamshwa, hasa kama hayuko sawa. Watu wanaomwamsha ni wale wenye ahadi naye,” alisema mlinzi huyo.

WEMA ATUMIWA MESEJI
Baada ya kuondoka nyumbani kwa Wema, Risasi Mchanganyiko lilimtumia ujumbe mfupi (SMS) ‘mreeefu’ wenye madai yote na ikaonesha ‘delivered’ kwenye simu ya Wema, lakini pia haikujibiwa.

TUNARUDI KWA CLEMENT  
Simu yake haikuwa ikipatikana hewani alipopigiwa ili na yeye apewe nafasi ya kusema lolote kuhusu sakata hilo.

MKE WA CLEMENT AVUNJA UKIMYA
Risasi Mchanganyiko liliamua kumsaka kwa simu ya mkononi mke wa Clement ambapo alipopokea na kusomewa mashitaka ya mumewe na nafasi yake kama shahidi muhimu alikiri hali ya jamaa kuwa tete kimfuko.
“Kuhusu hilo la nyumba ni kweli ilikuwa inadaiwa na benki (aliitaja jina) na walitaka kuinadi ili wapate fedha zao, lakini nikaingilia kati ili kulinda heshima ya familia.
“Unajua ile nyumba kuna mtu alituuzia, kwa hiyo Clement alitoa kiasi cha fedha lakini hakumalizia na akatumia hati ya nyumba kwenda kuombea huo mkopo. Kwa sababu benki walikuja juu nilitafuta mtu akainunua, kiasi cha fedha nikammalizia aliyetuuzia na kulipa benki,” alisema mwanamke huyo.

KUHUSU KUMFANYIA FITINA MUME AKAHAMISHWA KITENGO
Huyu hapa mke wa Clement: “Hilo si kweli bwana. Kwanza mimi ndiyo nilimfikisha pale alipofika. Sasa mtu nimuinue mwenyewe nitamfanyiaje fitina?
“Kwanza mimi siko naye siku hizi. Nilipoona anachukua magari ya nyumbani na kuyapeleka huko kwa nani sijui (Wema) nikaamua kukaa pembeni na kunyamaza kimya.
“Kama ni mabalaa anayapata hukohuko aliko, nisisingiziwe mimi kwa lolote lile.”
KUHUSU KUMWANDALIA FUMANIZI WEMA
“Aaa wapi! Nimwandalie fumanizi la nini? Yeye ana maisha yake mengine mimi niko na mambo yangu, muda huo sina kabisa, yaani niko bize sana,” alisema mwanamke huyo huku akidai muda huo alikuwa akidraivu.

PRODYUZA WA WEMA ALIJUA HILI?
Wiki mbili zilizopita, gazeti damu moja na hili, Ijumaa Wikienda liliandika katika ukurasa wake wa mbele habari yenye kichwa; MAGARI YA WEMA YAGEUZWA GESTI.
Katika habari hiyo, Wema alidaiwa kumtimua kazi prodyuza wake katika Kampuni ya Endless Fame, Rashid Mohammed ‘Chid Classic’ kwa sababu ya kumtuhumu kufanya ufuska kwenye magari yake maeneo ya Ufukwe wa Coco, Dar.
Siku chache mbele, prodyuza huyo alifunguka katika gazeti lingine pendwa ndani ya mjengo, Amani kuwa, Wema ‘amechoka’ siku hizi, halipi mishahara wafanyakazi wake na alitaka yeye awe kuwadi ndiyo wangeendana jambo ambalo yeye hakuwa tayari.
Baadhi ya habari zilizowahi kuandikwa na magazeti ya GPL kuhusu jeuri ya fedha ya Wema.
HABARI NYINGINE YA MJINI
Yapo madai kuwa, kutokana na maswahibu hayo ya kuwa kwenye wakati mgumu kifedha, kampuni yake imeanza kudoda na mbaya zaidi, marafiki zake anaokuwa nao kwenye raha, wamemkacha na kumwacha akihangaika mwenyewe.
“Msiniandike gazetini lakini ukweli ni kuwa, huu ndiyo wakati wake wa kujifunza kuchagua marafiki. Ona sasa, wale wote aliokuwa akila nao raha, wamekaa pembeni. Ni tatizo sawa, lakini pia ni funzo kwa upande mwingine,” alisema mpambe mmoja anayefanya naye kazi kwa karibu sana.


Source : GPL

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII