Maria Nyerere ambaye ni mke wa
aliyekuwa rais wa kwanza nchini Tanzania Mwalimu Nyerere, amesema Nelson
Mandela ataendelea kukumbukwa kwa moyo wake wa kusamehe na kumtaja
kwamba alikuwa ni zawadi ya dunia katika kuleta upendo na maridhiano.
Uhusiano kati ya familia ya Mwalimu Nyerere na
ile ya Mzee Nelson Mandela umekuwa ni wa karibu kiasi kwamba familia
yake inajiandaa kwenda kuhudhuria katika mazishi yatakayofanyika tarehe
15 mwezi huu.Awali mwandishi wetu Aboubakar Famau alizungumza na mama Maria, na kwanza alimuuliza jinsi gani amezipokea taarifa za msiba huo.
>>>>>>>BOFYA HAPA KUSIKILIZA SAUTI YAKE AKIELEZEA ALIVYOMJUA MANDELA<<<<<<
SOURCE : BBC
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII