Mwenyezi mungu alieumba aridhi na mbingu alimtofautisha
mwanadamu na wanya mnyama amepewa akili tuu bali mwanadamu amepewa akili na
utashi .Ila kwa hali ya sasa yale wanayofanya wanadamu ni kama wanatumia akili
tu bila utashi unyama matukio ya ajabu kimekuwa kitu cha kawaida sana kwa dunia
ya leo
Matukio ambayo zamani tulikuwa tukiyaona katika filamu ila
kwa sasa yanatokea katika jamii tulizopo inasikitisha na inahuzunisha sana
kuona mwanadamu mwenzio anapata maumivu yaliyosababishwa na mwanadamu mwenzie
Hivi karibuni hapa jiji mwanza mkazi mmoja wa Igoma
Aliefahamika kwa jina moja la Consolata amepigwa na mmewe na kung’atwa sikio na
mtu anaedaiwa kuwa ni hawara wa mumewe bi consolata amesema alikuwa akigombana na
mumewe ndipo hawara yake huyu alipokuja na musema ngoja tukuonyeshe maana
hutujui ndipo alipong’atwa sikio na kuondolewa sikio zima
Mara baada ya kufanyiwa ukatili huo alienda kulipoti katika
kituo cha polisi lakini kwa madai yake kuwa watuhumiwa waliachiwa kwakuwa
walikuwa wakijuana na baadhi ya askari waliokuwepo kituoni .Ndipo bi consolata
alipochukua hatua za kutafuta wasamalia wema kama waandishi ili waweze
kumsaidia aweze kupatiwa matibabu kwani ni mgeni jiji mwanza toka kigoma na
alikuja mwanza kwa ajili ya kumsalimu mumewe
Baada ya kuzungumza na waandishi alipelekwa kwenye taasisi
ya kivulini ambao mpaka sasa wanampatia huduma ya matibabu ukatili huu kiukweli
ni aibu kubwa kwa taifa letu
TUBADILIKE TUTAMBUE UTU WA MTU NDUGU ZANGU SHADDY CLASSIC TUNAKUPA POLE DADA CONSOLATA
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII