Pages

Monday, January 20, 2014

HII NDIO GARI MPYAA ALONUNUA DIAMOND, TAZAMA HAPA

 
 Hahaaaa kweli diamond noma sana, wanaosema ana hela kibao hawajakosea kabisa kwani kwa mafanikio aliyonayo na anaendelea kupata sidhani kama atafilisika leo. Najua kuna wengi mnaweza bisha na kusema kwani Mr Nice alikua wapi na leo yupo wapi, but ukweli ni kwamba Diamond na Mr Nice wanautofauti mkubwa katika kupanga na matumizi ya mshiko.

Hii si siri tena kua kwa sasa Diamond ndo anaongoza kwa kua msanii anaelipwa mshiko mrefu kuliko wote hapa bongo na nahisi anaelekea kua hata Afrika Mashariki. Nina ushahidi kidogo tu kua admin wenu wa Bongoclan nilipokua likizo katika jiji la Mwanza Diamond alipiga show katika jengo la Buzuruga Plaza na kulipwa shilingi Milioni 23. Sidhani kama kuna msanii yoyote wa bongo alishawahi kulipwa mshiko huo kwa show moja, ili afikishe mshiko huo nahisilazma apige kuanzia show 3 hadi 4 ili amfikie Damond.

Tuache Brabra na tuende kwenye utamu wenyewe, kama mnakumbuka miezi michache iliyopita msanii Diamond alinunua gari aina ya Toyota Prado na ilikua gumzo sana mtandaoni na kwenye magazeti ya udaku. Sasa baada ya mshiko kuongezeka kaamua kununua gari ambayo ni funiko yani hakuna msanii mwenye kiburi wala jeuri ya kununua gari hiyo. Maana akijaribu tu basi ujue uchumi wake utatetereka mbaya, nayo si nyingine ni Toyota Land Criser V8 Mpyaaaaaaaaaaaaaa.

Katika fukunyuafukunyua ya timu yetu ya Bongoclan tukagundua kua ili mtu aweze nunua gari hiyo ni lazima awe na dola za kimarekani 70,000 au ambayo ni zaidi ya milioni 110. Hakika ni gari ya ukweli sana na hapa bongo wanaotumia magari haya kwa wingi ni watu wenye vyeo vikubwa serikalini mfano JK, Pinda na baadhi ya mawaziri.

Timu nzima ya Bongoclan inapenda kumpongeza msanii Diamond kwa mafanikio aliyofikia kwani haijawahi kutokea hapa bongo msanii yeyote kumiliki gari ya aina hiyo na ya mkwanja mrefu kiasi hicho. Itakumbukwa kua marehemu kanumba aliwahi kumiliki V8 lakini hii ya Diamond ni noma sanaaaaaaa. Kweli Mziki unalipa hasa kama wasanii wa bongo wataichukulia kama kazi.


CREDITS: BONGOCLAN

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII