Pages

Thursday, January 30, 2014

SHILOLE AMUANIKA MCHUMBA AKE WA KIZUNGU, TAZAMA PICHA NA SOMA ALICHOKISEMA

KWA mara ya kwanza msanii wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amenaswa akiwa na mwanaume wa Kizungu anayedaiwa kuwa ndiye mchumba wake.
Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiwa na mchumba wake.
Chanzo makini kimepenyeza habari kuwa, safari za mara kwa mara za Shilole nchini Uingereza zimekuwa zikisababishwa na mchumba huyo wa Kizungu ambaye huwa anamuita kufurahia penzi lao pamoja na kumtafutia shoo mbalimbali.
“Ukweli ni kwamba Shilole ana mchumba wa Kizungu na walikutana kwenye shoo ya mara ya kwanza aliyoenda kufanya nchini Uingereza na hivi karibuni ataenda tena na amealikwa na huyo mchumba wake,” kilisema chanzo hicho.
Gazeti hili limekuwa la kwanza kunasa picha kadhaa za Shilole akiwa katika mapozi tofauti ya kimahaba na Mzungu huyo.
Baada ya chanzo hicho kumwaga ‘upupu’ huo, mapaparazi wetu walimtafuta Shilole ili aweze kufunguka ambapo bila kuumauma maneno, alikiri kuwa amepata mchumba huyo aliyemtambulisha kwa jina la Ankar.
Akizidi kumwaga data za boifrendi wake huyo, Shilole alisema awali walikutana kwenye moja ya shoo zake nchini humo ndipo urafiki ulipoota mizizi na kufikia hatua ya kuwa wapenzi.
“Kweli nina mchumba Mzungu ambaye ni raia wa Uingereza, nilipokuwa napataka nimefika, sipindui tena. Unajua muziki wangu na mauno yangu yanawavutia sana watu, siku ya kwanza aliniona kwenye shoo akanipenda ndipo tukaanzisha urafiki.
“Hivi karibuni nina safari ya kwenda nchini humo kwa mwaliko maalum alionipa, nitaenda peke yangu kwani safari nyingine zote zilizopita nilikuwa naenda na watu,” alisema Shilole.

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII