TAZAMA PICHA ZA MABASI YA MWENDO KASI YALIPOKUWA YAKIFANYIWA MAJARIBIO LEO MITAANI

0 comments


Mmoja ya basi la mwendo kasi likikatiza mtaa wa Lumumba ikiwa sehemu ya majaribio ya mabasi hayo ambayo yanaaminika yataondoa kabisa tatizo la usafiri katika jiji la Dar es Salaam.
CREDIT : GPL

Soma zaidi Hapa »

SHILOLE AMUANIKA MCHUMBA AKE WA KIZUNGU, TAZAMA PICHA NA SOMA ALICHOKISEMA

0 comments
KWA mara ya kwanza msanii wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amenaswa akiwa na mwanaume wa Kizungu anayedaiwa kuwa ndiye mchumba wake.
Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiwa na mchumba wake.
Chanzo makini kimepenyeza habari kuwa, safari za mara kwa mara za Shilole nchini Uingereza zimekuwa zikisababishwa na mchumba huyo wa Kizungu ambaye huwa anamuita kufurahia penzi lao pamoja na kumtafutia shoo mbalimbali.
“Ukweli ni kwamba Shilole ana mchumba wa Kizungu na walikutana kwenye shoo ya mara ya kwanza aliyoenda kufanya nchini Uingereza na hivi karibuni ataenda tena na amealikwa na huyo mchumba wake,” kilisema chanzo hicho.
Gazeti hili limekuwa la kwanza kunasa picha kadhaa za Shilole akiwa katika mapozi tofauti ya kimahaba na Mzungu huyo.
Baada ya chanzo hicho kumwaga ‘upupu’ huo, mapaparazi wetu walimtafuta Shilole ili aweze kufunguka ambapo bila kuumauma maneno, alikiri kuwa amepata mchumba huyo aliyemtambulisha kwa jina la Ankar.
Akizidi kumwaga data za boifrendi wake huyo, Shilole alisema awali walikutana kwenye moja ya shoo zake nchini humo ndipo urafiki ulipoota mizizi na kufikia hatua ya kuwa wapenzi.
“Kweli nina mchumba Mzungu ambaye ni raia wa Uingereza, nilipokuwa napataka nimefika, sipindui tena. Unajua muziki wangu na mauno yangu yanawavutia sana watu, siku ya kwanza aliniona kwenye shoo akanipenda ndipo tukaanzisha urafiki.
“Hivi karibuni nina safari ya kwenda nchini humo kwa mwaliko maalum alionipa, nitaenda peke yangu kwani safari nyingine zote zilizopita nilikuwa naenda na watu,” alisema Shilole.

Soma zaidi Hapa »

MAMA WEMA ATANGAZA VITA NA DIAMOND, SOMA HAPA DUUH

0 comments

HABARI mpya! Mama wa Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu, Mariam Sepetu anadaiwa kuingia rasmi mitaani akiwasaka wapenzi, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Wema, chanzo cha uhakika kimesema na Amani. 

Wema na Diamond wakiwa katika pozi la kimahaba.
 Kwa mujibu wa chanzo hicho makini, mama Wema ameamua kuchukua uamuzi huo baada ya kusikia taarifa kutoka kwa watu kwamba, Diamond amekuwa akisambaza maneno mitaani kuwa haogopi vitisho vya mwanamke huyo kufuatia hatua yake ya kumrudia binti yake.

 ILIKUWAJE KWANI?
Hivi karibuni, mama Wema alizungumza na gazeti tumbo moja la hili, Ijumaa Wikienda linalotolewa na Kampuni ya Global Publishers Ltd kila siku ya Jumatatu na kusema kitendo cha Diamond kumrudia bintiye hakubaliani nacho.

 Aliongeza kuwa, kufuatia hatua hiyo iko siku ataingia mtaani kumsaka Diamond na popote pale atakapomnasa, atamkata na panga.
Mama Wema, Mariam Sepetu anayewasaka wapenzi hao.
 TURUDI KWA CHANZO
“Jamani si mnakumbuka juzikati mama Wema alisema atamsaka Diamond? Sasa amesikia Diamond anatangaza mitaani kwamba, hatishiki na tamko la mama mkwe wake huyo na watakapokutana watajua nani zaidi.

 “Hivi ninavyosema, mama Wema ameingia mtaani kuwasaka. Lengo lake awakute wote wawili ili awaanzishie timbwili la kufa mtu.
 “Tangu Ijumaa iliyopita, kila siku anatoka kwenda mitaani kuwasaka, naamini siku akiwakuta pamoja kweli itakuwa vita kubwa,” kilisema chanzo chetu.
Gari la Wema na la Diamond yakiwa yameegeshwa nyumbani kwa Wema.
 KWA NINI ASIENDE NYUMBANI?
Chanzo kilipoulizwa kama kweli mama Wema amepania kuwanasa wawili hao, kwa nini asiwafuate nyumbani kwa binti yake, Kijitonyama, Dar ambako wanapika na kupakua, kilijibu:

 “Ameweka mtego wake pale, bahati mbaya sana Diamond naye anaishi kwa machale. Kuna siku anakwenda kulala kuna siku haendi. Huenda na yeye (Diamond) ameweka watu wake ndani kwa Wema wa kumpelelezea kama mama Wema atakwenda au ana dalili za kwenda.”
 Chanzo kikaendelea: “Siku hizi Diamond anaweza kwenda kwa Wema, akaacha gari lake na kutoka na la Wema na kurudi kwake usiku sana.”
Paparazi wa GPL akiwa nyumbani kwa Diamond.
 AMANI LAWASAKA WAHUSIKA
Baada ya kuzinyaka nyeti hizo, Amani liliamua kuutafuta ukweli ambapo Jumanne iliyopita lilimsaka mama Wema kwa njia ya simu lakini iliita bila kupokelewa.
Amani lilitumia simu zake mbili kumpigia mwanamke huyo.

 Baada ya dakika tano, mama huyo mwenye ‘machungu’ na mwanaume yeyote anayemchezea bintiye alituma ujumbe mfupi wa maneno (SMS) akisema: Nipo msibani tuma sms. Pia akatuma sms kwenye simu ya pili akisema: Nipo msibani, ulikuwa unasemaje?
 Amani lilimtumia madai yote kuhusu yeye kuanza kuwatafuta Wema na Diamond, pia likamjulisha kwamba kama anawatafuta kweli, muda huo, wawili hao walikuwa wapo chumbani kwa Wema hawajaamka.
 Hata hivyo, mama Wema hakujibu meseji yoyote kati ya hizo mbili hali iliyotafsiriwa na Amani kuwa, uchungu wa msiba ulimuondolea uwezo wa mawasiliano.
Paparazi wa GPL akiongea na mlinzi wa Wema nyumbani kwake.
 NYUMBANI KWA DIAMOND
Mapaparazi wetu walitia timu nyumbani kwa Diamond, Sinza-Mori na kukutana na mtu mmoja aliyedai ni mjomba wa staa huyo ambaye alidai Diamond Platnumz alitoka asubuhi na mama yake, Sanura Kassim kwenda Tegeta, Dar.

 NYUMBANI KWA WEMA
Baada ya kutoka nyumbani kwa Diamond huku wakiamini Mbongo Fleva huyo kaenda Tegeta kama alivyosema mjomba mtu, mapaparazi walikwenda nyumbani kwa Wema.
Baada ya kugonga geti kwa dakika moja, alitokea mlinzi na mambo yalikuwa kama ifuatavyo;
Paparazi: Mambo?

Wema.
 Mlinzi: Poa, karibu.
Paparazi: Asante, nina shida na Wema, sijui nimemkuta?
Mlinzi: Wamelala, hawawezi kuamka muda huu.
Paparazi: Wamelala? Nani na nani?
Mlinzi: Madam (Wema) na Diamond.

 Paparazi: Ina maana Diamond yumo ndani?
Mlinzi: Si nimekwambia wamelala?
Paparazi wetu alifanikiwa kupenyeza macho kwenye nafasi ya uzio na kuyaona magari ya wote wawili, la Diamond aina ya Toyota Land Cruiser V8 na la Wema, Toyota Lexus Harrier.

Soma zaidi Hapa »

HIVI NDIVYO M4C ILIVYOKULA VICHWA MOROGORO, AFANDE SELE NAYE ALIHUTUBIA

0 comments

Halima Mdee: Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Mtibwa, katika mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika jana.
Mbowe na Afande Sele: Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akimtambulisha mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Afande Sele, wakati wa mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Dama, uliofanyika katika Kata ya Tungi mjini Mororgoro jana.
Afande Sele: Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Afande Sele akiwahutubia wananchi wa Kata ya Tungi mjini Morogoro jana, katika mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoj Daima, ambao pia ulihutubiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe.
Mbowe, Halima wakiondoka Ifakara: Mwenyekiti wa Chama cha Demokreasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee wakiondoka baada ya kuhutubia mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika mjini Ifakara jana.
Mkutano Ifakara: Maelefu ya wakazi wa mji wa Ifakara, wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, ambao ulihutubiwa na Mweneyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jana.
Mabango Ifakara: Baadhi ya wananchi mji wa Ifakara wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali, wakati wa mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima, ambao ulihutubiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe jana.

Wananchi Ifakara: Sehemu ya maedlfu ya wakazi wa mji wa Ifakara, wakitawanyika baada ya mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima, ambao ulihutubiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe jana.
(Picha na JF)

Soma zaidi Hapa »

HII NDIO GARI MPYAA ALONUNUA DIAMOND, TAZAMA HAPA

0 comments
 
 Hahaaaa kweli diamond noma sana, wanaosema ana hela kibao hawajakosea kabisa kwani kwa mafanikio aliyonayo na anaendelea kupata sidhani kama atafilisika leo. Najua kuna wengi mnaweza bisha na kusema kwani Mr Nice alikua wapi na leo yupo wapi, but ukweli ni kwamba Diamond na Mr Nice wanautofauti mkubwa katika kupanga na matumizi ya mshiko.

Hii si siri tena kua kwa sasa Diamond ndo anaongoza kwa kua msanii anaelipwa mshiko mrefu kuliko wote hapa bongo na nahisi anaelekea kua hata Afrika Mashariki. Nina ushahidi kidogo tu kua admin wenu wa Bongoclan nilipokua likizo katika jiji la Mwanza Diamond alipiga show katika jengo la Buzuruga Plaza na kulipwa shilingi Milioni 23. Sidhani kama kuna msanii yoyote wa bongo alishawahi kulipwa mshiko huo kwa show moja, ili afikishe mshiko huo nahisilazma apige kuanzia show 3 hadi 4 ili amfikie Damond.

Tuache Brabra na tuende kwenye utamu wenyewe, kama mnakumbuka miezi michache iliyopita msanii Diamond alinunua gari aina ya Toyota Prado na ilikua gumzo sana mtandaoni na kwenye magazeti ya udaku. Sasa baada ya mshiko kuongezeka kaamua kununua gari ambayo ni funiko yani hakuna msanii mwenye kiburi wala jeuri ya kununua gari hiyo. Maana akijaribu tu basi ujue uchumi wake utatetereka mbaya, nayo si nyingine ni Toyota Land Criser V8 Mpyaaaaaaaaaaaaaa.

Katika fukunyuafukunyua ya timu yetu ya Bongoclan tukagundua kua ili mtu aweze nunua gari hiyo ni lazima awe na dola za kimarekani 70,000 au ambayo ni zaidi ya milioni 110. Hakika ni gari ya ukweli sana na hapa bongo wanaotumia magari haya kwa wingi ni watu wenye vyeo vikubwa serikalini mfano JK, Pinda na baadhi ya mawaziri.

Timu nzima ya Bongoclan inapenda kumpongeza msanii Diamond kwa mafanikio aliyofikia kwani haijawahi kutokea hapa bongo msanii yeyote kumiliki gari ya aina hiyo na ya mkwanja mrefu kiasi hicho. Itakumbukwa kua marehemu kanumba aliwahi kumiliki V8 lakini hii ya Diamond ni noma sanaaaaaaa. Kweli Mziki unalipa hasa kama wasanii wa bongo wataichukulia kama kazi.


CREDITS: BONGOCLAN

Soma zaidi Hapa »

KWELI PESA HULETA HESHIMA, TAZAMA VOGUE MPYA ALONUNUA LADY JAY DEE....

0 comments

Heshima pesa, shikamoo makelele. Congrats Jide.
CREDITS : JESTINA GEORGE!! ONE LOVE

Soma zaidi Hapa »

BREAKING NEWS : KIKWETE ATANGAZA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI, HAYA NDIO MAJINA YA BARAZA JIPYA, BOFYA HAPA

0 comments

Mabadiliko Baraza la Mawaziri 2014


Soma zaidi Hapa »

VIOJA : TAZAMA PICHA ZA SHINDANO LA MISS JELA, WAFUNGWA WAKICHUANA KUMPATA MISS WAO

1 comments


HAYA ni mashindano ya urembo yanayofanyika kila mwaka katika moja ya gereza la wafungwa huko nchini Brazil, waliyoanzisha mashindano haya wanasema wanawapa haki wafungwa nao wajisikie kama binadamu na si kama wanyama kwani muda mwingi wanakuwa wanafanya kazi kwahiyo inakuwa sio mbaya kuwapa muda kidogo wajifurahishe katika mioyo yao na sio muda wote waonekane watumwa wa kazi. Mshindi wa taji hilo anapewa uangalizi na zawazi za kutosha kutoka kwa waandaaji wa shindano hilo.











Soma zaidi Hapa »
Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs