Pages

Saturday, February 23, 2013

WARAKA KWA WATANZANIA : "MAAJABU, MAAJABU, MAAJABU X 20"

Imeandikwa na  Omwilili Tayebwa, UDSM
 
Tanzania ni nchi yenye vivutio vingi.Vivutio gani hivyo,?Ni vivutio vya utalii.Watalii wengi wa ndani na nje ya nchi,wanapenda sana ,tena kutoka kwenye vitako vya mioyo yao,kushuhudia jinsi dhana ya ujinga inavyoandaliwa ,kutengenezwa hatimae kupakuliwa kama chakula.Matokeo ya kidato cha nne,mwaka wa masomo 2012/2013,  yamefanya watalii waongezeke ghafla nchini humu. Fuatilia rekodi za watalii walioingia tokea tarehe kumi na saba hadi leo mwezi huu.Tatizo la kushindwa kwa wadogo wetu si kwa sababu yao katika asilimia kubwa. Serikali yetu chini ya Chama tawala mnachokijua, inapungukiwa yafuatayo: AIBU,HOFU YA MUNGU,HURUMA NA AKILI TEKELEVU(Practiacal intelligency). Mwaka huu ni wa pekee kweli.  Halii hii imekuwa ikitokea huko nyuma lakini si kwa furaha na vifijo kama mwaka huu!. Hata wanyama wengine yaani hayawani wamenotisi jambo hili.Hivi simba na twiga wasiodhuriwa na risasi wakichana mbuga kwa kukasirikia jambo hili,tutakimbilia wapi ili tunusuru roho zetu. Ndugu zangu , KUNA MAANA YOYOTE YA KUENDELEA KUIMBA WIMBO WA TANZANIA NAKUPENDA,nakupeeeeendaaaaaaaaaaa!
Ni uwenda wazimuuuu!!!!Usiasa umefunika utekelezaji.Zaidi ya nusu ya watainiwa,wamezungusha(MAANA YAKE WANA SIFURI AU ZERO KWA KIINGEREZA)!!!!Eheheeeeeeeeheeee!!!! Utasikia mipango mizuri serikalini ya kupeleka miradi ya maendeleo katika sehemu fulafulani nchini, TANGU LINI MTU HASIYE NA ELIMU MBADALA AHUSISHWE KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI AU MRADI HUO? UKWELI NI KWAMBA, FEDHA ZIKITENGWA KWA MIRADI HIYO, HIZO NI KWA AJILI YA WAHUSIKA WALIOTUMWA NA SERIKALI , WASIO NA HAYA  WAENDE WAZITAFUNE. INAMAANARAIA WAKIPATA ELIMU, DILI LITAVUNJIKA NA UFISADI UNANYIMWA NJIA, KWANI UFISADI NI MOJAWAPO YA VYANZO VIKUU VYA KUKUSANYA PASIPO KUTAWANYA KWA BAADHI YA VIONGOZI KTK NJE NA NDANI YA SERIKALI!! . JIULIZE,KUSHINDWA KWA WANAFUNZI KWA KUSHANGAZA ,KUMEANZA LEO? KWANINI HAKUNA MSHTUKO NA UTEKELEZAJI CHANYA KUTOKA SERIKALINI,KWANI NDIYO YENYE KUPANGA BAJETI?. IMEJIKITA KATIKA USIASA BADALA YA VITENDO CHANYA.EBU ONJA YATOKEOAYO BUNGENI,KAMA SEHEMU YA SERIKALI , KIDOGO . 
KAMBI YA UPINZANI BUNGENI IKIFURUKUTA,CHAMA TAWALA KINATOA TAARIFA YA UONGO,KURA ZA MIKONO ZINAAMRIWA NA ANA MAKINDA,WENGI WAPE NDO LINAKUWA SULUHISHO LA MGOGORO.Hata mbuzi hawawezi kuendesha BUNGE LAO,kwa namna hii!!!. KAMA NDUGU YANGU ULIFUATILIA MVUTANO WA UWEPO WA CURRICULUM YA ELIMU HAPA NCHINI,HUKO BUNGENI,HUTAONA TOFAUTI KWA MTIRIRIKO WA WARAKA WANGU,KAMA UNA UWEZO WA KUPAMBANUA NA HUCHUKII UKWELI.Ningeishauri serikali la kufanya, ila sijui kama ina blogi inayokusanya na kuheshimu mawazo ya raia wake.Serikali yetu ina imani kwamba raia wake ni wajinga na imeisha jenga dhana ya dharau. Bahati mbaya, si hivyo,ililenga kutumia kanuni hiyo kule Mtwara, mambo yaliwatokea puani ,mwaka huu.Cha ajabu sana,mtu mmoja akitokezea,kiushauri au kuipinga serikali,akiwa na mawazo endelevu,shukrani yake ni kuambulia risasi ya moto,na tetesi za kifo chake zitatolewa kwamba , KAUAWA NA WATU WASIOFAHAMIKA.Mi nahisi Tanzania inaweza kuonja vita ya ndani miaka ijayo......

1 comment:

  1. Hatuhitaji nidhamu ya woga au chuki dhidi ya ukweli kuweka wazi mambo haya, kwa kuwa tayari yapo katika serikali yetu. Tuzidi kupigana kwa falsafa ya namna hii kwa kuwa bado tunadhaniwa kama watu wa chini, ila ipo siku, our ACTIONS WILL SPEAK LOUDER THAN WORDS!

    ReplyDelete

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII