BUNGE LAKUBALI KUJADILI HOJA BINAFSI ZA MNYIKA NA NASSARI....PATA HABARI KAMILI HAPA
Wabunge wawili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia
CHADEMA, Mh Joshua Nassari na Mh John Mnyika, kwa nyakati tofauti
wameujulisha umma kupitia akaunti zao za mtandao wa Kijamii kuwa Bunge
limekubali kuingiza kwenye ratiba hoja zao binafsi kuhusu maswala mawili
tofauti, moja ni kuhusu ubora wa elimu nchini na nyingine kuhusu maji
safi na maji taka kwa jiji la Dar es Salaam.
Katika
bandiko la Mh Joshua Nassari
ameandika “Leo Bunge limeridhia kuingiza katika ratiba ya shughuli za
bunge Hoja yangu Binafsi kuhusu mwenendo wa Baraza la mitihani la Taifa
unavyohathiri Elimu ya Tanzania. Kama Taifa linalohitaji kupiga hatua ni
lazima tuangalie upya mfumo wa elimu na Baraza la mitihani na mdau
muhimu kwa kuwa baraza ndilo Lenye mamlaka ya kutunga, kusimamia na
kusahihisha mitihani yote nchini Tanzania isipokuwa kwa vyuo vikuu”
Nae Mh Mnyika katika
bandiko
lake ameandika “Hatimaye leo Bunge limekubali kuingiza katika ratiba za
bunge hoja yangu binafsi juu ya Maji (safi na taka). Hoja hii itaipa
bunge zima fursa ya kujadili na kupitisha maazimio ya hatua za haraka za
kuboresha upatikanaji wa Maji Safi na kushughulikia Maji Taka katika
jiji zima la Dar es Salaam.
Mengine mengi yaliyomo ndani ya hoja hii nitaendelea kuwadokeza.Tatizo
la maji (safi na taka) ni letu sote kila mwananchi wa jiji la Dar. Hivyo
tuungane na kuhakikisha tunaweka maslahi ya umma kwanza!”
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII