Wabunge wawili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Mh Joshua Nassari na Mh John Mnyika, kwa nyakati tofauti wameujulisha umma kupitia akaunti zao za mtandao wa Kijamii kuwa Bunge limekubali kuingiza kwenye ratiba hoja zao binafsi kuhusu maswala mawili tofauti, moja ni kuhusu ubora wa elimu nchini na nyingine kuhusu maji safi na maji taka kwa jiji la Dar es Salaam.
Katika bandiko la Mh Joshua Nassari ameandika “Leo Bunge limeridhia kuingiza katika ratiba ya shughuli za bunge Hoja yangu Binafsi kuhusu mwenendo wa Baraza la mitihani la Taifa unavyohathiri Elimu ya Tanzania. Kama Taifa linalohitaji kupiga hatua ni lazima tuangalie upya mfumo wa elimu na Baraza la mitihani na mdau muhimu kwa kuwa baraza ndilo Lenye mamlaka ya kutunga, kusimamia na kusahihisha mitihani yote nchini Tanzania isipokuwa kwa vyuo vikuu”
Nae Mh Mnyika katika bandiko lake ameandika “Hatimaye leo Bunge limekubali kuingiza katika ratiba za bunge hoja yangu binafsi juu ya Maji (safi na taka). Hoja hii itaipa bunge zima fursa ya kujadili na kupitisha maazimio ya hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa Maji Safi na kushughulikia Maji Taka katika jiji zima la Dar es Salaam.
Mengine mengi yaliyomo ndani ya hoja hii nitaendelea kuwadokeza.Tatizo la maji (safi na taka) ni letu sote kila mwananchi wa jiji la Dar. Hivyo tuungane na kuhakikisha tunaweka maslahi ya umma kwanza!”
Pages
▼
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII