Pages

Friday, November 9, 2012

SHILOLE ADAI KUSUMBULIWA SANA NA WASAGAJI...WENGINE NI MASTAA WENZIE

 
MUIGIZAJI anayeng’ara katika muziki wa Bongo Fleva huku akidili pia na mambo ya filamu, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amefunguka kuwa anasumbuliwa sana na wadada wanaojihusisha na tabia ya usagaji kitu ambacho kinamkera.

 Akizungumza na Gazeti la Ijumaa hivi karibuni, Shilole alisema anawashangaa wasichana wanaomtokea na kumtaka kimapenzi na akaeleza kuwa kinachomuuma zaidi ni kwamba kuna wengine ni mastaa wenzake.
“Yaani wananisumbua sana, mbaya zaidi wengine ni wasichana maarufu sana lakini hawana hata aibu, wakiendelea kunisumbua nitayaweka majina yao hadharani, mimi sipendi kabisa tabia hiyo,” alisema Shilole.

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII