Pages

Saturday, March 16, 2013

KAMA ULIKUWA HUJAIONA LIST YA WANAMUZIKI 10 MATAJIRI SANA AFRICA NDIO HII HAPA

Kwa mujibu wa mtanado wa answerafrica, Hii ndiyo Top 10 ya wanamuziki tajiri zaidi Afrika;
10. Jose Chameleone

Amezaliwa mwaka 1979 Kijisehemu cha mali za kifahari anazomiliki ni Range, Cadillac Escalade, Mercedes Benz ml 200 super custom convertible, Premio. Anamiliki jumba la kifahari huko Uganda - Seguka hills pembeni kidogo ya jiji la Kampala pamoja na ardhi na nyumba sehemu nyingine.

9. Banky W
Jina lake halisi ni Olubankole Wellington kutoka Naijeria, alizaliwa March 27, 1981 huko Marekani, alianza kuimba kanisani kablaya kuingia katika muziki wa Dunia,ana dili kadhaa ikiwepo kubwa kabisa na kampuni ya Samsung katika kutangaza bidhaa zake ndani ya soko la Naijeria, Ni muanzilishi na mmiliki wa mfuko wa hisani wa Mr capable foundation;ambao husaidia watoto walio katika mazingira magumu kupata elimu.

8. Hugh Masekela
Alizaliwa April 4, 1939, Jina lake kamili ni Hugh Ramopolo Masekela kutoka Afrika Kusini, mbali na vyanzo vyake vingine vya mapato, anamiliki Studio ya kisasa kabisa ya muziki huko Botswana, na kutokana na jina kubwa utaalam na umaarufu wake kutoka muziki wake, Huzunguka dunia nzima kutumbuiza katika matamasha makubwa kabisa ya kimataifa.

7. 2 Face Idibia
Jina lake halisi ni Innocent Ujah Idibia mwanamuziki, mwandishi wa nyimbo pamoja na mwigizaji filamu maarufu ana albam 5 na tuzo 40 tofauti mpaka sasa, Amewekeza pesa zake katika kumiliki nyumba na viwanja huko Naijeria, dau lake limewekwa wazi kuwa huwa analipwa dola 50000 mpaka 80000 kwa onyesho moja, anamiliki ukumbi wa atarehe maarufu pamoja na biashara nyingine ndogondogo.

6. Fally Ipupa
Fally Ipupa, Mwanamuziki na mwandishi wa nyimbo kutoka Kongo, Mbali na muziki Fally pia ana dili nono la kutoklezea katika matangazo ya kampuni kubwa kabisa ya mavazi huko Ufaransa.

5. Salif Keita
Salif Keïta, mzaliwa wa mali, alizaliwa 25th of August, 1949, inatajwa kuwa msanii huyu anamiliki Kisiwa pamoja na ardhi maeneo kadha wa kadha huko Ufaransa. 

4. Koffi Olomide
Koffi Olomide, jina lake halisi ni Antoine Christophe Agbepa Mumba, alizaliwa July 13, 1956, Koffi huchaji hadi euro 100,000 kwa show.

3. D’banj
Dapo Daniel Oyebanjo maarufu kama Koko Master ama D’banj, alizaliwa June 9, 1980).

D banj ni mwanamuziki wa kwanza kabisa kutoka Afrika kusainiwa katika lebo ya Kanye west - GOOD music label, Mbali na kuwa mtu wa karibu wa Rais wa Naijeria, Mhe. Goodluck Jonathan, huyu pia anamiliki Night Club, anafanya biashara ya maji, ana nyumba Naijeria na pia huko Atlanta Marekani. Dau lake kwa show linatajwa kufikia dola 100000.

2. P-Square

Peter na Paul, Mbali na dili kali na mtandao maarufu wa mawasiliano huko Naijeria, wanatajwa kujiingiza katika biashara ya mafuta, Wana majumba ya kifahari na dau lao kwa show sasa linatajwa kufikia dola 150000. 

1. Youssou N’dour
Youssou N’Dour kutoka Senegal, alizaliwa October, 1959. Ni mfanyabiashara na pia mwanasiasa, Anamiliki vituo kadhaa vya TV na Radio huko Senegal pia na ana mashamba na majumba yenye thamani kubwa.

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII