Pages

Thursday, March 7, 2013

KING MAJUTO AFICHUA SIRI ZA KUANGUKA KWA FILAMU ZA VICHEKESHO

MCHEKESHAJI nguli hapa nchini, Amri Athuman ‘King Majuto’ ameweka wazi kuwa, wasambazaji wa kazi za sanaa wamechangia kwa kiasi kikubwa kuyumba kwa soko la filamu za vichekesho.

King Majuto aliyasema hayo jijini Dar es Salaam, katika mazungumzo maalum na Saluti5 juu ya maoni aliyonayo kuhusiana na maendeleo ya filamu za Komedi hapa nchini.

“Unajua, unaweza kuandaa komedi yako kwa hata zaidi ya milioni 7, lakini unapompelekea msambazaji anataka kuinunua kwa milioni 2,” alisema King Majuto.

King Majuto alisema kuwa, kutokana na hilo, waandaaji wengi hivi sasa wamekuwa wakitayarisha kazi zao katika kiwango kisichokidhi, ili kuepuka gharama na hasara na matokeo yake mashabiki wanafikia hatua ya kuzipuuza na kuzikimbia kazi zao.

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII