KING MAJUTO AFICHUA SIRI ZA KUANGUKA KWA FILAMU ZA VICHEKESHO
MCHEKESHAJI
nguli hapa nchini, Amri Athuman ‘King Majuto’ ameweka wazi kuwa,
wasambazaji wa kazi za sanaa wamechangia kwa kiasi kikubwa kuyumba kwa
soko la filamu za vichekesho.
King
Majuto aliyasema hayo jijini Dar es Salaam, katika mazungumzo maalum na
Saluti5 juu ya maoni aliyonayo kuhusiana na maendeleo ya filamu za
Komedi hapa nchini.
“Unajua,
unaweza kuandaa komedi yako kwa hata zaidi ya milioni 7, lakini
unapompelekea msambazaji anataka kuinunua kwa milioni 2,” alisema King
Majuto.
King
Majuto alisema kuwa, kutokana na hilo, waandaaji wengi hivi sasa
wamekuwa wakitayarisha kazi zao katika kiwango kisichokidhi, ili kuepuka
gharama na hasara na matokeo yake mashabiki wanafikia hatua ya
kuzipuuza na kuzikimbia kazi zao.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII