Pages

Friday, March 15, 2013

KUTANA NA MSICHANA WA MIAKA 22, ALIYEANDIKA HOTUBA YA USHINDI RAIS MTEULE WA KENYA .......NI MDOGO SANA LAKINI ANA UPEO WA HALI YA JUU

Julie Wang'ombe ni msichana wa miaka 22 tu lakini tayari amejijengea jina kubwa. Bi. Wang'ombe ndiye aliyeandika hotuba ya ushindi wa Rais mteule Uhuru Kenyatta, aliyoitoa siku ya Jumamosi katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki Afrika Mashariki. Pia, Julie alitoa sala maalum kwa Rais mteule siku hiyo.

Julie anajulikana sana kwa kipaji cha kuandika mashairi, na hilo aliligundua mnamo 2009 kwenye concert ya Slam Afrika iliyofanyika huko Westlands, Nairobi. Baadae mwaka huo, alipomaliza shule ya sekondari ya Hillcrest, Julie alienda kusoma katika chuo kikuu cha Duke cha Marekani.

Wakati akiwa Duke, alikutana na washairi kadhaa wazoefu na bora, mmoja wao akiwa ni Joshua Benne, ambaye ndiye aliyemhamasisha zaidi.

Leo, Julie ana uwezo wa ku-perfom kama mshairi kwa watazamaji duniani kote.

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII