Kampuni kubwa na inayoongoza kwa utengenezaji na
usambazaji wa filamu nchini, Steps entertainment, wanajiandaa kwa ajili
ya tamasha la filamu nchini litakalofanyika mwezi ujao kwenya viwanja
vya leaders jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mwandishi wa habari. mmoja wa waandalizi wa
tamasha hilo alisema kuwa lengo kubwa la tamasha ni kukuza na kuendeleza
tasnia ya filamu Tanzania na pia kuwapongeza wasanii walofanya vizuri
katika mwaka 2012.
Aliongeza kwa kusema kuwa tamasha hilo litahusisha wadau wote wa
bongomovies nchini na ndani ya nchi na amewataka wananchi kujitokeza
kwa wingi siku ya tamasha hilo ambayo tarehe yake itatangazwa rasmi
kwenye vyombo vya habari ili kwa pamoja waweza kusherekea mafanikio
ambayo tasnia ya filamu nchini inaendelea kuyapata.
Pia siku steps enternatinment watamuenzi marehemu Steven kanumba
kwa mchango wake mkubwa katika kuendeleza na kukuza tasnia ya
bongomovies nchini.
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII