Picha aliyoweka Wema Sepetu Instagram kuelezea ugomvi uliotokea, na
kuandika: ” Da fight I got into today caused me da marks I hav on my
baq… things I do for da people I love always cost me… nd u knw wat ama
kip doin.”
Staa huyo wa Bongo Movie ambaye pia ni mmilikiwa kampuni ya Endless
film, amemfikisha mama yake mzazi anayejulikana kama Miriam Sepetu
kwenye Kituo cha Polisi Kijitonyama jijini Dar es salaam kwa madai ya
kwenda nyumbani kwake na kufanya vurugu zilizosababisha kuharibika kwa
samani nadani ya nyumba yake.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita, nyumbani kwa Wema, Kijitonyama, jijini Dar.
Mbali na mama mtu, wengine waliofikishwa kituoni hapo ni dada mkubwa
wa Wema aitwaye Nuru na kijana aliyefahamika kwa jina moja la Bestizo
ambaye inasemekana ni mshirika mkubwa wa Diamond kwenye masuala ya
mtandao wa msanii huyo.
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII