KAMATI Kuu ya Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) itakutana kwa siku
mbili kwenye kikao chake cha kawaida jijini Dar es Salaam, kuanzia tarehe 3-4 Aprili, 2013.
Katika kikao hicho cha
siku mbili, Kamati Kuu itajadili pamoja na mambo mengine, yatokanayo na kikao kilichopita, hali ya kisiasa nchini, pia itapokea taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya kikao cha Baraza Kuu kilichofanyika mwezi Februari mwaka huu, ikiwemo mpango wa uendeshaji chama kwa
kanda.
Aidha, Kamati Kuu pia
itajadili mpango kazi na bajeti ya Chama kwa
mwaka 2013-2014
Imetolewa leo tarehe
Aprili 2, 2013, Dar es Salaam
na;
Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa
Habari CHADEMA
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII