Pages

Wednesday, April 3, 2013

TAZAMA PICHA ZA TUKIO LA VURUGU ZILIZOTOKEA TUNDUMA, HAKIKA TANZANIA IMECHAFUKA SASA



Hii ndiyo hali halisi ya Mji mdogo wa Tunduma leo kuanzia asubuhi

Matairi yanachomwa katikati ya barabara

Mambo hayo 



Mwandishi wetu pamoja na waandishi wenzake walipata shida sana kufika mji wa Tunduma walikutana na vikwazo vingi sana lakini wananchi walikuwa waelewa waliwasaidia kutoa magogo na matairi ili wapite wakapate habari












Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Diwani akiongea na waandishi wa habari
Wanafunzi wakisindikizwa na jeshi la polisi kurudi majumbani mwao
Polisi wakiendelea na kazi yao katika mitaa ya Tunduma
Baadhi ya magari ya IT yaendayo nchini Zambia yakiwa yamepakiwa nnje kidogo ya mji wa Tunduma kuogopa kuharibiwa kwa magari hayo

----------------
Diwani wa kata ya Tunduma Ndugu Frank Mwaijoka (Chadema) pamoja na mchungaji wa kanisa la KKT katika eneo hilo la Tunduma wilayani momba Mkoani mbeya wametakiwa kujisalimisha kituo cha Polisi Tunduma mara baada ya kuhusika na uchochezi wa kidini hali ambayo imepelekea kutokea kwa vurugu  katika eneo hilo.

Vurugu hizo zimeanza majira ya saa 4 asubuhi katika eneo hilo la tunduma mara baada ya kundi la watu wanaodai kuwa wao ni wafuasi wa dini ya kikristo wakidai waruhusiwe kuchinja mifugo na kuuza katika mabucha yao hali iliyo pelekea kuibuka kwa vurugu hizo.

Akizungumza kuhusiana na tukio hilko Kamanda wa Polisi Mkoani humo Ndugu Diwani Athumani amesema kuwa kufuatia kuwepo kwa tukio hilo jumla ya watu zaidi ya 40 tayari wamekwisha kamatwa .

Amesema mpaka sasa taarifa walizo zipata kufuatia vurugu hizo zinaeleza kuwa miongoni mwa watu walichochea vurugu hizo ni diwani wa kata hiyo ya Tunduma Ndugu John Mwaijoka pamoja na Mchungaji wa kanisa la kkt ndugu Neema Mwaipusa ambao kwa pamoja wametakiwa kujisalimisha kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi.

Amesema suala hilo limegubikwa  na siasa kwani tayari viongozi wa serikali akiwemo Mkuu wa mkoa huo Ndugu Abbas Kandoro amekwisha litolea ufafanuzi Apri 02 mwaka huu wakiwepo pia viongozi wa dini .
Amesema kwa asilimia kubwa mgogoro huo juu ya nani achinje umeingiliwa na mambo ya kisiasa kwani hata baadhi ya wananchi wa maeneo hayo wamekuwa wakilalamika juu ya kutokea kwa vurugu hizo.

Amesema shughuli za kibiashara katika eneo hilo zimeshindwa kufanyika katika eneo hilo hivyo kufanya wananchi kupata adha hasa kwa nchi jirani ya Zambia ambao kwa asilimia kubwa wanategema kupata mahitaji kutoka mpakani mwa Tanzania.

Hata hivyo Diwani amesema kuwa katika vurugu hizo askari mmoja  pamoja na mwananchi wamejeruhiwa kwa kupigwa mawe ambapo tayari wamekwisha fikishwa kituo cha polisi.

Kufuatia hali hiyo Kamanda huyo wa Polisi amesema kwa sasa hali imelejea katika hali yake ya kawaida hivyo amewataka wananchi wa maeneo hayo kuwa watulivu wakati jeshi hilo la Polisi likiendela na msako wa kuwatafuta wahalifu wengine.

1 comment:

  1. kila mtu achinje kwa imani yake na mabucha yaandikwe. kama ni ya waislamu yajulikane na ya wakristo pia. si vizuri kuongozwa na imani ya mtu mwingine

    ReplyDelete

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII