Pages

Friday, April 19, 2013

WABUNGE WA CCM WAPANGA KUMNG'OA NDUGAI....MWENYEWE ASEMA NI FITNA ZA SITTA KWA VILE ALIUKOSA USPIKA


Kwa taarifa za uhakika kutoka kwa mwandishi wa habari aliyeko Dodoma, anasema wabunge wa CCM hasa wale wanaojulikana kama wapambanaji wa ufisadi na wengine,wamekuwa na vikao juzi, jana na leo asubuhi wamekubaliana kuwa ni lazima aondoke kwenye unaibu spika kwa vile amekuwa akitumia jazba badala ya kuzingatia kanuni kwa vile hakuna kanuni inayomruhusu spika kumfungia vikao 5 papo kwa papo.

Pia wanadai amewaharibia mkakati wao ambao walikwisha upanga wa kumfungia Lema kufuatia tuhuma za kumsema Rais kuwa ni mdini, wanadai akifungiwa tena ataonekana anaonewa na hivyo kumpandisha juu kisiasa, kilichowaudhi ni pale walipomwita na hakwenda kuwasikiliza zaidi ya kuwaambia kuwa yupo bize na hakuna kanuni iliyovunjwa, pia akasikika akisema kuwa hizo ni fitna za Sitta kukosa uspika.

Leo wamekubaliana kupeleka azimio lao kwa Pinda na Jenister Mhagama kwa hoja kuwa Ndugai kwa kutumia jazba bila kufuata kanuni anasabisha chama kionekane dhaifu kuwa kinaogopa wapinzani hivyo kukifanya kidharauliwe na kuchukiwa na jamii.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa maazimio yamewekwa kwa maandishi na wamechaguliwa watu wawili kuyapeleka mbele.

Mchakato unaendelea tusubiri tuone.



No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII