Msuya anayemiliki vitega uchumi kadhaa mkoani Arusha na Manyara amepigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakati akitokea Mererani katika migodi ya madini ya Tanzanite majira ya saa 6.30 mchana jana.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo kutoka uwanja wa ndege wa KIA ambao hawakuwa tayari kutajwa majina yao, mfanyabishara huyo baada ya kuuawa hakuna kitu kilichochukuliwa katika gari yake.
‘’Hawa jamaa walimvizia njia ya panda ya Mirerani na KIA na walifanikiwa kumsimamisha na ghafla alitokea mtu akiwa katika usafiri wa pikipiki na kummiminia risasi nyingi na inaonekana alikufa popo hapo’’alisema mtoa habari huyo.
(Picha na Swahilitz.com)
Duu! Dunia imekwisha amakweli ukiwa na mali watu Jicho kwako kuzuia Maendeleo Huku wakisahau Kuwa Duniani Tunapita tu! R. I. P Msuya.
ReplyDelete