Alipotoka
kwenye jumba la Big Brother Africa, mwakilishi wa Ghana, Selly mwezi
uliopita aliahidi kumchukulia hatua za kisheria Ammy Nando kwa kusambaza
habari ya uongo kuhusu yeye.
Wiki mbili baada ya Nando kuondolewa kwenye shindano hilo, Selly amebadilisha mawazo yake.Kwenye mahojiano ya na gazeti linalouza
zaidi nchini Ghana, Graphic Ghana,Selly amesema hana mpango wa kumshtaki
tena Nando kwakuwa Mungu ameingilia kati na kumpigania.“Hapana, sitachukua hatua zozote za
kisheria dhidi ya Nando sababu Mungu amejibu sala zangu na ameniokoa.
Ameipigania vita yangu, na leo Afrika nzima imekuja kufahamu Nando ni
mtu wa aina gani na hiyo ni hukumu tosha kwangu.Tangu nimereja, nimekuwa nikimuomba
Mungu kuingilia kati na kurudisha heshima yangu lakini kwa njia yake
mwenyewe Mungu, amenionesha mimi ni mwenye haki.Hata kabla Nando hajatolewa, niliambiwa
na waandaji wa Big Brother nisichukue hatua yoyote ya kisheria dhidi
yake na nilijiuliza ni vipi nitasafisha jina langu na kurekebisha
heshima yangu iliyoharibiwa lakini Mungu alikuwa na mipango yake kwangu.
Huo ulikuwa ni mchezo wa Nando kuniondoa kama mshindani mwenye nguvu
lakini Mungu anayejua zaidi hakuniweka kwenye aibu,”alisema Selly.
Selly amesema ingawa hajasikia chochote
kutoka kwa Nando baada ya kuondolewa, hakuwa tayari kukubali ombi lake
la msamaha kama angemuomba.
“Sitamsamehe kamwe Nando kwa si tu
kunidhalilisha mimi na familia yangu, nchi yangu na mpenzi wangu
aliyeumizwa na maneno na fedheha muda wote huo. Ameniletea madhara
makubwa kwenye heshima yangu na kile alichokifanya
hakistahimiliki,”alisema.
“Kinachoumiza zaidi ni kwamba, sikuwa na
fursa ya kujitetea mwenyewe humo kwasababu sikusikia chochote kile
hadi pale nilipotoka na niliumizwa zaidi kwasababu sikujua jinsi mpenzi
wangu alivyojisikia, niliporudi nyumbani nashukuru amekuwa nguzo imara
nyuma yangu.”
Kwa sasa, Selly, ambaye jina lake halisi
ni Selorm Galley yupo chini ya usimamizi wa kampuni ya ARV Media na
yupo tayari kuingia tena kwenye uigizaji wa filamu
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII