JOKATE AELEZA SIRI YA KUFUATWA NA WANAUME.....SOMA ZAIDI

MREMBO anayefanya vizuri katika mambo mengi nchini, Jokate Urban Mwegelo (pichani) ametaja sababu nne zinazowafanya wanaume kumzimikia, akiwemo nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Akiandika katika mtandao wake wa Kidoti Life Style, Jokate, mshindi wa pili wa Miss Tanzania 2006, alizitaja sababu hizo kuwa ni kujiamini, kujitegemea, kupendeza na tabasamu muda wote.
“Kujiamini ndiyo sababu kubwa ya kwanza inayonifanya nipendwe zaidi, hamna kitu kinachowavutia watu hasa wanaume kama kujiamini,” anaandika Jokate.
“Kujitegemea ni sababu ya pili, binafsi naamini kwamba hakuna kitu kinachowaboa wanaume kama mwanamke ambaye anapenda vitu vya kupewa. Ukimuonesha mwanaume wewe unapenda kutafuta vyako, basi jua atakupenda zaidi.”
Jokate alisema sababu nyingine inayomfanya kuwa kivutio kwa wanaume ni kupendeza katika mavazi, hasa kwa kuvaa nguo zenye rangi ya kuonekana.
Sababu nyingine aliyoitoa ni tabasamu, akiweka wazi kuwa tabasamu linamfanya aonekane mrembo zaidi.
Gazeti hili liliwasiliana na Jokate kuhusiana na maandiko hayo ambaye alijibu; “Hahaha….sina comment hapo aisee…”
Jokate pia ni mwanamitindo, msimamizi wa shughuli mbalimbali katika kampuni yake ya Kidoti iliyozinduliwa mwaka jana.

SOURCE : GPL
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs