MREMBO anayefanya vizuri katika mambo mengi nchini, Jokate Urban
Mwegelo (pichani) ametaja sababu nne zinazowafanya wanaume kumzimikia,
akiwemo nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Akiandika
katika mtandao wake wa Kidoti Life Style, Jokate, mshindi wa pili wa
Miss Tanzania 2006, alizitaja sababu hizo kuwa ni kujiamini,
kujitegemea, kupendeza na tabasamu muda wote.
“Kujiamini ndiyo sababu
kubwa ya kwanza inayonifanya nipendwe zaidi, hamna kitu kinachowavutia
watu hasa wanaume kama kujiamini,” anaandika Jokate.
“Kujitegemea ni
sababu ya pili, binafsi naamini kwamba hakuna kitu kinachowaboa wanaume
kama mwanamke ambaye anapenda vitu vya kupewa. Ukimuonesha mwanaume wewe
unapenda kutafuta vyako, basi jua atakupenda zaidi.”
Jokate alisema
sababu nyingine inayomfanya kuwa kivutio kwa wanaume ni kupendeza katika
mavazi, hasa kwa kuvaa nguo zenye rangi ya kuonekana.
Sababu nyingine aliyoitoa ni tabasamu, akiweka wazi kuwa tabasamu linamfanya aonekane mrembo zaidi.
Gazeti hili liliwasiliana na Jokate kuhusiana na maandiko hayo ambaye alijibu; “Hahaha….sina comment hapo aisee…”
Jokate pia ni mwanamitindo, msimamizi wa shughuli mbalimbali katika kampuni yake ya Kidoti iliyozinduliwa mwaka jana.
SOURCE : GPL
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII