MWENYEKITI Mtendaji wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, wameingia katika mzozo mzito kuhusu uwekezaji katika sekta ya gesi.TANZANIA DAIMA WANAYO HABARI NZIMA.ENDELEA KUISOMA KWA KUBONYEZA HAPA.
Katika mzozo huo, Mengi amemshambulia Waziri Muhongo kwa kumwita ni mwongo, mpotoshaji na mwenye lengo la kuwatoa Watanzania kwenye hoja ya msingi ya rasilimali yao ya gesi.
Mengi alitoa kauli hiyo jana kupitia taarifa yake aliyoisambaza kwenye vyombo vya habari mbalimbali nchini.
Mzozo wa vigogo hao ulianza wiki mbili zilizopita baada ya Mengi ambaye pia ni Mwenyekiti wa taasisi ya Uwekezaji nchini (TPSF), kukutana na waandishi wa habari na kueleza msimamo wa taasisi hiyo katika suala la uwekezaji wa gesi nchini.
Katika maoni yake, TPSF ilisisitiza umuhimu wa ushirikishwaji wa Watanzania katika uchumi wa gesi na kuishauri serikali kusitisha ugawaji wa vitalu vya gesi hadi sera ya gesi itakapokuwa tayari na taasisi hiyo iliomba kukutana na Waziri Muhongo kwa majadiliano zaidi.
Baada ya ushauri huo, Waziri Muhongo alijibu kupitia vyombo vya habari kwamba mpango wa kugawa vitalu vya gesi na kuingia mikataba uko palepale kama ulivyopangwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Prof. Muhongo pia alitamka bila kumng’unya maneno kwamba hana mpango wa kukutana na TPSF, kwani kufanya hivyo ni kupoteza muda, na kuongeza kuwa uwezo wa wafanyabiashara wa Tanzania ni kuwekeza kwenye soda na juisi, si kwenye sekta ya gesi.
Septemba 7, mwaka huu, mzozo huo uliingia katika hatua mbaya zaidi baada ya mtu aliyejitambulisha kwa jina la ‘CCM Tanzania’, kusambaza taarifa kwa njia ya barua pepe kwa vyombo vyote vya habari na kumshambulia Mengi kwa kumwita fisadi, mbinafsi na mfitini wa maendeleo.
Pages
▼
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII