UNAFAHAMU KUWA HAWA NDIO WASANII WENYE HESHIMA ZAIDI HAPA TZ????

Kutokana na utafiti uliofanywa na timu nzima ya the choice, imebaini wasanii 6 upande wa muziki wa kizazi kipya wanaoheshimika sana Tanzani katika jamii.Vigezo vilivyo zingatiwa katika utafiti huu ni pamoja na kutobaini skendo za ajabu ajabu kwa hawa wasanii,pia hutumiwa katika utoaji nasaa mbalimbali katika jamii pia wanajiheshimu katika mambo yao kwa ujumla. 


1.LADY JAY DEE 



Mwanadada JIDE ama binti machozi ameweza kuongelewa sana kama msanii anayeheshimika sana tanzania kutokana na idadi kubwa ya watu walio hojiwa kumtaja yeye kama ndo mwana muziki mwenye kuheshimika sana tanzania kwa upande wa muziki wa kizazi kipya 


2.PROF J
Prof J naye hakuwa nyuma katika kutajwa na idadi kubwa,Prof j kama muhasisi mkubwa wa huu muziki wa kizazi kipya anaheshimika sana kutokana na mchango wake mkubwa katika hii gemu bila ya kuwa na sifa mbaya zinazo weza kumchafulia heshima yake 
3.FID, Q
HUYU ni msanii aliyezungumziwa kuwa ni mpole sana mkinywa na hufanya kazi zake kwa umakini mkubwa,Ni mtu apendaye kufikiri jambo kwa umakini sana kabla ya kulitenda,Pia kazungumziwa sana na idadi kubwa ya walio hojiwa 
4.A.Y
AY kati ya mchakalikaji mkubwa na mpenda maendeleo katika kazi zake, ni kijana anaye ibeba nembo ya Tanzania katika ngazi ya kimataifa,Kujiheshimu kwake na kuto kuwa na skendo pamoja na kuchakalika kwake kunamfanya aonekane kuwa mtu wa kuigwa kwa vijana wengine.
5.MWANA FA
Binamu ama waweza sema pacha wa A.Y kutokana na kuwa na urafiki wa karibu sana na wa muda mrefu na A.Y.MWANA FA pia katajwa kwa idadi kubwa ya wadau kama mtu anayeheshimika sana nchini hasahasa katika nyanja hii ya muziki wa kizazi kipya.
 6. JUMA NATURE

Juma Nature ama kiroboto, ni mtu asiye penda makuu pia kazungumziwa kama mtu anayependa kuona watu wote wakiwa sawa na  hapendi kuona manyanyaso kwa watu wengine sababu ya kuto kuwa na uwezo.

Wamemtaja kama mtu mwenye nyota ya kupendwa sana na watu kwani yaonyesha anaweza akakaa hata miaka kadhaa bila ya kutoa wimbo wowote ila pindi apandapo tu jukwaani watu hufarijika hata aimbapo nyimbo za zamani.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs