Kutokana
na utafiti uliofanywa na timu nzima ya the choice, imebaini wasanii 6
upande wa muziki wa kizazi kipya wanaoheshimika sana Tanzani katika
jamii.Vigezo vilivyo zingatiwa katika utafiti huu ni pamoja na kutobaini
skendo za ajabu ajabu kwa hawa wasanii,pia hutumiwa katika utoaji nasaa
mbalimbali katika jamii pia wanajiheshimu katika mambo yao kwa ujumla.
1.LADY JAY DEE
Mwanadada JIDE ama binti machozi ameweza kuongelewa sana kama msanii anayeheshimika sana tanzania kutokana na idadi
kubwa ya watu walio hojiwa kumtaja yeye kama ndo mwana muziki mwenye
kuheshimika sana tanzania kwa upande wa muziki wa kizazi kipya
2.PROF J
Prof
J naye hakuwa nyuma katika kutajwa na idadi kubwa,Prof j kama muhasisi
mkubwa wa huu muziki wa kizazi kipya anaheshimika sana kutokana na
mchango wake mkubwa katika hii gemu bila ya kuwa na sifa mbaya zinazo
weza kumchafulia heshima yake
3.FID, Q
HUYU ni
msanii aliyezungumziwa kuwa ni mpole sana mkinywa na hufanya kazi zake
kwa umakini mkubwa,Ni mtu apendaye kufikiri jambo kwa umakini sana kabla
ya kulitenda,Pia kazungumziwa sana na idadi kubwa ya walio hojiwa
4.A.Y
AY kati
ya mchakalikaji mkubwa na mpenda maendeleo katika kazi zake, ni kijana
anaye ibeba nembo ya Tanzania katika ngazi ya kimataifa,Kujiheshimu
kwake na kuto kuwa na skendo pamoja na kuchakalika kwake kunamfanya
aonekane kuwa mtu wa kuigwa kwa vijana wengine.
5.MWANA FA
Binamu ama waweza sema pacha wa A.Y kutokana na kuwa na urafiki wa karibu sana na wa muda mrefu na A.Y.MWANA FA pia katajwa kwa idadi kubwa ya wadau kama mtu anayeheshimika sana nchini hasahasa katika nyanja hii ya muziki wa kizazi kipya.
6. JUMA NATURE
Juma
Nature ama kiroboto, ni mtu asiye penda makuu pia kazungumziwa kama mtu
anayependa kuona watu wote wakiwa sawa na hapendi kuona manyanyaso kwa
watu wengine sababu ya kuto kuwa na uwezo.
Wamemtaja
kama mtu mwenye nyota ya kupendwa sana na watu kwani yaonyesha anaweza
akakaa hata miaka kadhaa bila ya kutoa wimbo wowote ila pindi apandapo
tu jukwaani watu hufarijika hata aimbapo nyimbo za zamani.
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII