Show ya kihistoria inayosubiriwa na wengi kufanyika ndani ya viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam leo, tayari jukwaa litakalotumiwa na wasanii wanne kutoka hapa nyumbani na wale wakali wa kulishambulia jukwaa barani Afrika P~Square lipo katika maandalizi ya mwisho mwisho pamoja na kufunga mziki.
Wasanii watakao-perform jukwaa moja na P` Square ni Malkia wa Bongo fleva mwenye miaka kumi na tatu kwenye gemu Lady Jay Dee a.k.a Anaconda, King wa R&B Ben Paul, mwamba wa kaskazini Joh Makini na MC shupavu au Heavy weight Mc au Daddy Joseph Haule wa Mitulinga Mchawi wa Rhymes.
CREDIT: VIJIMAMBO BLOG
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII