James Kisaka enzi za uhai wake.
Aliyekuwa kocha wa makipa wa Klabu ya Simba, James Kisaka amefariki
dunia leo asubuhi katika Hospitali ya Burhan, Dar es Salaam. Kisaka
aliyewahi kuwa kipa wa timu hiyo miaka ya nyuma, alikuwa akisumbuliwa na
maradhi ya kichwa, macho na miguu kwa muda mrefu. Global Publishers
tunatoa pole kwa ndugu na jamaa.
MUNGU AIPUMZISHE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI. AMINA
SOURCE: GPL
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII