Nora amefunguka kupitia kipindi cha Filamonata cha 100.5 Times Fm na kudai kuwa Ray amekuwa akimbania hata kwenye baadhi ya makampuni ambayo anapeleka kazi zake.
“Mpaka kwenye kampuni ambayo nimepeleka kazi nimeshawahi kusikia wanasema, wakaniahidi sana mpaka nikawakubalia walichokuwa wanataka wao. Lakini yeye (Ray) alitanguliza movies zake, akasema ana movie zake sijui kitu gani..” amelalamika Nora.
Ameeleza kuwa Ray amewahi kumbania kufanya kazi na marehemu Kanumba, na hata Mtitu sababu ikiwa ile ile kumkataa kimapenzi.
“Alishawahi..kitu ambacho kwangu kimeshawahi, sasa mimi sijui yeye ni alivyo au kwangu..ila mimi alinibania kwa sababu nilikuwa simtaki, akaniharibia kwa Mtitu. Kanumba kipindi kile alikuwa anamsikiliza sana Ray, akamwambia asifanye kazi na mimi. Hata Kanumba alikuwa ameelewana na mimi Ray akamwambia ‘achana naye’.” Nora ameiambia Filamonata.
Amedai kuwa wanaume wengi katika tasnia ya filamu wanamekuwa wanawanyanyasa wanawake kwa kuwata kimapenzi, na kwamba inakuwa ni mambo ya ndani ambayo sio rahisi kufahamika.
“Ikitokea hivyo inakuwa ni mambo ya ndani sana kiasi kwamba hata mwenzako anakwambia kwamba utaona kama utaendelea kuwa flani.” Nora amefunguka.
Nora amedai kuwa ana kazi nyingi lakini ameshindwa kuziingiza sokoni kwa sababu ya kubaniwa.Hata hivyo Nuru Nassoro aka Nora amesema ameshasamehe na anaendelea na kazi zake.
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII