HUU NDIO WASIFU WA PAPA MPYA, SOMA HISTORIA YAKE HAPA
Jorge Bergolio alizaliwa katika mji wa Buenos Aires huko
argentina, ni mtoto kati ya familia ya watoto wa tano. Wazazi wake walihamia
argentina na baba yake Mario Jose
Bergogio alikuwa mfanyakazi wa kampuni ya reli na mama yake Regina Sivori
alikuwa mama wa nyumbani tu.. katika enzi za utoto wake papa francis aliwahi
kutolea pafu moja kutokana na mtatizo ya kiafya aliyokuwa nayo.
Elimu Yake
Elimu yake yote aliipata huko argentina na alihitimu shahada
ya uzamili ya Chemia katika chuo kikuu cha Buenos Aires kabla ya kuamua kuendelea na masomo ya
seminari. Alianza maisha ya kimtumikia Mungu tarehe 11 march 1958.
Kabla ya kuwa papa
Alipewa daraja la upadri tarehe 13 december 1969 na askofu
mkuu Ramon Jose Castellano kabla ya kuendelea na masomo ya thiolojia katika
chuo cha San Miguel huko Buenos Aires ambako alipata elimu yake mpaka kufikia
daraja la kuwa proffesa wa theolojia
Kutokana na utendaji wake mzuri wa kazi, Bergoglio alikuwa
akipandishwa madaraja mpaka kuwa Gombera (rector ) wa seminari ya San Miguel ambapo alihudumia mpaka 1986.
Bergoglio alipewa daraja uaskofu msaidizi wa Buenos Aires
mwaka 1992 na alisimikwa rasmi kuwa askofu
wa Auca mwezi June 1992, daraja hilo alipewa na kardinali Antonio
Quarracino ambaye alikuwa ndio askofu mkuu wa Buenos Aires. Baadae mwaka 1998
mwezi february, alichukua kiti cha
Uaskofu mkuu wa Buenos Aires alichoachiwa na kardinali Antonio Quarracino
Ukardinali
Mwezi february tarehe 21,
Bergoglio alipewa ukardinali na papa yohane wa II, akitambulika kama
Cardinal Mchungaji wa San Roberto Bellarmino. Akiwa kardinali, alichaguliwa
kuongoza katika nyadhifa mbalimbali katika baraza la makardinali huko Roma (Roman
Curia)
Katika ukardinali wake, Bergoglio alitambulika kwa kuwa mtu
mwenye kujali sana utu, mwenye msimamo kuhusu maswala ya imani, pia ni mtu
aliyekuwa mtari wa mbele kusimamia haki za kijamii. Anajulikana pia kwa sifa ya
unyenyekevu na asiyependa maisha makuu kwani mpaka anakuwa kardinali huko
Argentina alikuwa hana gari na alikuwa anatumia usafiri wa umma kumfikisha
sehemu alizokuwa akihitaji kwenda.
Daraja la Upapa
Cardinali Bergoglio alichaguliwa hapo jana tarehe 13 March,
2013 siku ya pili baada ya mchakato wa kumtafuta papa kuanza hapo tarehe 11
march, 2013. Mara tu baada ya kuchaguliwa alichagua jina la Francis I jina
alilochukua kutoka kwa mtakatifu Francis wa Assisi
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII