Pages

Thursday, March 14, 2013

HUU NDIO WASIFU WA PAPA MPYA, SOMA HISTORIA YAKE HAPA

 
Jorge Bergolio alizaliwa katika mji wa Buenos Aires huko argentina, ni mtoto kati ya familia ya watoto wa tano. Wazazi wake walihamia argentina na baba yake  Mario Jose Bergogio alikuwa mfanyakazi wa kampuni ya reli na mama yake Regina Sivori alikuwa mama wa nyumbani tu.. katika enzi za utoto wake papa francis aliwahi kutolea pafu moja kutokana na mtatizo ya kiafya aliyokuwa nayo.
 
Elimu Yake

Elimu yake yote aliipata huko argentina na alihitimu shahada ya uzamili ya Chemia katika chuo kikuu cha Buenos Aires  kabla ya kuamua kuendelea na masomo ya seminari. Alianza maisha ya kimtumikia Mungu tarehe 11 march 1958.




Kabla ya kuwa papa
Alipewa daraja la upadri tarehe 13 december 1969 na askofu mkuu Ramon Jose Castellano kabla ya kuendelea na masomo ya thiolojia katika chuo cha San Miguel huko Buenos Aires ambako alipata elimu yake mpaka kufikia daraja la kuwa proffesa wa theolojia

Kutokana na utendaji wake mzuri wa kazi, Bergoglio alikuwa akipandishwa madaraja mpaka kuwa Gombera (rector ) wa seminari ya  San Miguel ambapo alihudumia mpaka 1986. 


Bergoglio alipewa daraja uaskofu msaidizi wa Buenos Aires mwaka 1992 na alisimikwa rasmi kuwa askofu  wa Auca mwezi June 1992, daraja hilo alipewa na kardinali Antonio Quarracino ambaye alikuwa ndio askofu mkuu wa Buenos Aires. Baadae mwaka 1998 mwezi  february, alichukua kiti cha Uaskofu mkuu wa Buenos Aires alichoachiwa na kardinali Antonio Quarracino

Ukardinali
Mwezi february tarehe 21,  Bergoglio alipewa ukardinali na papa yohane wa II, akitambulika kama Cardinal Mchungaji wa San Roberto Bellarmino. Akiwa kardinali, alichaguliwa kuongoza katika nyadhifa mbalimbali katika baraza la makardinali huko Roma (Roman Curia)

Katika ukardinali wake, Bergoglio alitambulika kwa kuwa mtu mwenye kujali sana utu, mwenye msimamo kuhusu maswala ya imani, pia ni mtu aliyekuwa mtari wa mbele kusimamia haki za kijamii. Anajulikana pia kwa sifa ya unyenyekevu na asiyependa maisha makuu kwani mpaka anakuwa kardinali huko Argentina alikuwa hana gari na alikuwa anatumia usafiri wa umma kumfikisha sehemu alizokuwa akihitaji kwenda.

Daraja la Upapa
Cardinali Bergoglio alichaguliwa hapo jana tarehe 13 March, 2013 siku ya pili baada ya mchakato wa kumtafuta papa kuanza hapo tarehe 11 march, 2013. Mara tu baada ya kuchaguliwa alichagua jina la Francis I jina alilochukua kutoka kwa mtakatifu Francis wa Assisi

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII