Amani Golugwa Katibu wa Chadema – Kanda ya Kaskazini
Kufuatia tamko lililotolewa jana tarehe 11 Machi 2013 huko musoma
na Mwenyekiti wa chama Mhe Freeman A. MBowe (MB), ambalo ni msisitizo wa
tamko lililotolewa wiki kadhaa zilizopita huko mbeya la azimio la
kutaka waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi na naibu wake
kuwajibika kufuatia matokeo mabaya ya mitihani ya kidato cha NNE,
CHADEMA kanda ya Kaskazini inaunga kwa mkono tamko hilo ambalo limebeba
utashi wa wananchi ambao ni wazazi wa vijana wetu ambao kwa sababu ya
mfumo mbovu wa elimu, umeendelea kupelekea matokeo kuwa mabaya na hasa
ya mwaka na yenye kuleta fedheha na kilio kikubwa sana kwa taifa letu.
Ieleweke kuwa hili ni janga na serikali kwa ukiziwi wake wa
kutosikiliza sauti za watu itajikuta ikiingia kwenye gharama kubwa ya
kukabiliana na kundi kubwa la vijana waliopo mtaani ambao hawana jambo
la kufanya kwa sababu mfumo wa elimu umewafanya kuwa washindwaji kwa
kiwango ambacho hawataweza kujimudu kimaisha.
Hili si jambo dogo hata kidogo, tafsiri ya matokeo mabaya haya
inawalenga moja kwa moja mawaziri wenye dhamana na pasifanyike masihara
wala mizaha kuhusu jambo hili la kufeli huku kwa vijana wetu. Kauli zao
za awali zimeonyesha wao kutojali na kulitia umaanani kwa kutoa
vijisababu visivyo na mashiko wakati wao ndio wenye dhamana. Ni dhahiri
kuwa takwimu za elimu zimeshuka kutoka aslimia 89.3 ya mwaka 2005 hadi
kufika asilimia 34.5 kwa mahesabu haya kiwango cha elimu kimeporomoka
kwa asilimia 54.8 (Chanzo: Hotuba ya Waziri Mkuu akizungumza na waandishi wa habari tarehe 2 Machi 2013).
Takwimu hii inazungumza mambo mengi, maana yake ni kuwa mfumo mbovu
unaosimamiwa na Chama Chama Mapinduzi kwa asilimia hii 54.8 ya vijana
wetu watakuwa wamewezeshwa tu kujua kusoma kwa mashaka, kuandika na
kuhesabu kwa shida kitu ambacho hakitawasaidia kupambana na changamoto
za kimaisha iwapo hawataweza kupata fursa za kujiendeleza kwa ziada.
Hili ni janga kubwa na wahusika ni lazima wawajibike maana ni dhahiri
kwa mfufulizo wa kuporomoka huku ni dhahiri wameshindwa kusimamia elimu
ya Tanzania.
CHADEMA kanda ya kaskazini, tunawaalika wazazi wote na vijana wetu
wote ambao wamekuwa wahanga wa matikeo haya mabovu siku ya tarehe 25
Machi 2013 kushiriki katika maandamano haya ya kushinikiza kuwajibika
kwa waziri elimu na mafunzo ya ufundi stadi na naibu wake. Zaida ya hapo
ni kuitaka pia serikali kufanya utaratibu wa kuwajibika kuwasaidia
vijana hawa katika kushughulikia janga hili. Aidha katika kuanzisha
vituo vya masomo kuwawezesha kusoma ili kurudia mitihani au lolote
litakaloonekana lenye msaada. Maamuzi mabaya ya hamaki na yasiyo ya
kujali katika jambo hili yataweza kuzaa kizazi kibovu ambacho kitakuwa
ni mavuno ya matunda ya maamuzi yetu yasiyoonyesha utashi wa kujali ya
sasa.
Nawaomba wazazi wote katoka mikoa ya Tanga, Kilmanjaro, Arusha na
Manyara wafike katika ofisi za chama za wilaya zilizopo katika mikoa yao
au ofisi za wabunge (CHADEMA) kuandikisha majina yao na ya watoto wao
ili kupata idadi kamili. Siku ya tarehe 25 Machi kuanzia SAA NNE asubuhi
kuanzia mahali ambao tutawajulisha kutakuwa na maandamano makubwa
katika JIJI la Arusha yatakayokuwa na ujumbe huu na yatawashirikisha
viongozi wote wa chama, wabunge wote kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini,
wadau wa elimu, taasisi zisizo za kiserikali zenye kujishughulisha na
masuala ya elimu pamoja na watanzania wote ambao kwa dhati ya moyo
wameguswa na matokeo haya mabaya ya elimu, wazazi na vijana wote
waliopatwa na janga hili.
Taarifa nyingine zitawajia kama ambavyo tutawajulisha kupitia vyombo vya habari na ofisi za wabunge na makatibu wa majimbo.
Niwaombe Watanzania wote wakazi wa kanda ya Kaskazini tujitokeze
kwa wingi katika maandamano haya ya AMANI yatakayofanyaika katika JIJI
la Arusha na tuonyeshe Utanzania wetu na tuonyeshe kuwajali watoto wetu.
SIKU YA MAANDAMANO NJOO NA KITAMBAA CHEUPE MKONONI.
Imetolewa leo tarehe 12 Machi 2013.
Ofisi ya Kanda ya Kaskazini
Amani Golugwa
Katibu – Kanda ya Kaskazini
+255 754 912 914
golugwa@gmail.com
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII