MGOMO WA WALIMU UMEIVA

Mgomo wa walimu uliotangazwa na Raisi wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian Mukoba ambao umeanza leo tarehe 30 Julai, 2012 umeshika kasi katika sehemu mbalimbali hapa nchini kwa kushuhudia katika baadhi ya Mikoa walimu wakitii tamko la Chama Chao, Kutokana na mgomo huo Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kupitia kwa Waziri wa Elimu Bw. Shukuru Kawambwa imetoa tamko kwa walimu wote kusitisha mgomo na kurudi kazini mara moja,
tamko ambalo limepingwa na walimu wakidai kuwa mgomo wao ni halali na umefuata taratibu zote hivyo hawatarejea kazini mpaka pale serikali itakapotimiza matakwa yao ambayo ni kuongezewa mshahara kwa asilimia 100% , kupata posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu, posho ya walimu wa masomo ya sayansi (55%) na walimu wa masomo ya sanaa(50%) pamoja na kulipwa madai ya malimbikizo yao ya mishahara.
Hali hii imepelekea kuwe na hali inayotia shaka katika tasnia nzima ya elimu kwani kuna baadhi ya walimu wachache ambao hawauungi mkono mgomo huu kitendo ambacho kinatafsiriwa kuwa ni usaliti kwa walimu walio wengi. Serikali ikitoa kitoa tamko kupitia Waziri wa elimu imewataka walimu hao waendelee na moyo huohuo wa unaoitwa wa “kizalendo” na kwamba serikali inawahakikishia usalama wao endapo kutakuwa na vitisho vyovyote dhidi yao.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs