Seif Shaban ‘Matonya’.
Na Mwandishi WetuWAKATI wasanii wa Bongo Fleva,
Elias Barnaba na Estalina Sanga ‘Linah’ wakidaiwa kupokea fedha na
kuitolea mbavuni shoo ya Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ au Jide,
msanii Seif Shaban ‘Matonya’ naye ameuvaa msala mpya wa kuikacha shoo
hiyo huku akiminyia mshiko wa kianzio (advance) aliolipwa tangu
mwishoni mwa Aprili, mwaka huu.
Kwa mujibu wa mtandao wa Lady Jaydee,
Matonya alikuwa miongoni mwa wasanii watakaopafomu katika shoo ya
kuadhimisha miaka 13 ya Lady Jaydee inayotarajia kufanyika Mei 31, mwaka
huu katika Ukumbi wa Nyumbani Lounge, jijini Dar lakini baadaye
akagaili.
Kwenye maelezo ambayo Jide ameyaweka katika mtandao wake,
aliainisha madai kuwa huenda Matonya naye akawa ametumiwa na watu
wasioitakia mafanikio shoo hiyo baada ya kupata taarifa kuwa anatarajia
kutumbuiza kwenye shoo hiyo kama ilivyotokea kwa Barnaba na Linah.
Kudhihirisha
hilo, Lady Jaydee ameanika mahojiano kati ya Gardner G. Habash
‘Captain’ kama meneja wa Lady Jaydee na Matonya kwenye blogu yake
kuonesha namna ambavyo anahisi staa huyo ametumiwa. Yafuatayo ni baadhi
ya mahojiano haO:
Matonya: Kaka kumbe tarehe ni lini kumbe?
Captain: Ni Ijumaa tar 31 Mei 2013 kaka mwezi ujao. Tutakuwa na Linah, Jay, Barnaba, Matonya, TID, Hamza Kalala.
Matonya: Kaka kumradhi sana kuimba na bendi kwa sasa sitoweza manake
mtahitaji mandalizi makubwa ili nifanye kazi vizuri ningeomba nitizamwe
katika kazi nyingine kaka kumradhi sana.
Captain: Duh! nilishatangaza kaka, lakini sawa. Je, nitapata ile hela nilipe wengine ndugu yangu?
Matonya: Aisee! hata nimekosa raha kukujuza ili swala bro, kesho saa
tano nitampa yule rafiki yangu anaitwa Pizon walikuja kuleta ile pesa
ya gari kwa hiyo wataileta hapo hapo ofisini.
Captain: Sawa kaka usijali, nitashukuru akiileta ili huku nisipate lawama.
Matonya: ok bro.
Mara kimyaaaaaaa... baada ya siku mbili tatu maongezi yakaendelea
Captain: Naam kaka, mzigo haujaletwa. Tafadhali ileteni tu hiyo hela
ya watu kaka. Napewa lawama, isitoshe we ni ndugu yangu usikubali hela
ndogo iharibu.
Matonya: Gadner haiwezi kuwa hivyo, kuna mapungufu kidogo nayaweka sawa uipate. Kumradhi sana blaza.
Captain: Asante
Pamoja na kukubaliwa kutoshiriki shoo hiyo kutokana na sababu
alizojitetea, Matonya bado hajarejesha fedha za kianzio alizolipwa kwa
ajili ya shoo hiyo hali ambayo inaleta mtafaruku mwingine licha ya kuwa
alisisitizwa kurejesha.