SOMA KUHUSU MBUZI HUYU WA AJABU...ANABAKA WANAWAKE N.K

UKISTAAJABU ya Musa utaona ya Firauni. Mbuzi wa ajabu ajulikanaye kwa jina la ‘Mawimbi’ anafanya vitu ambavyo kwa akili za kibinadamu unaweza usiamini, Amani linamwanika mwanzo mwisho. Mbuzi huyo anayemilikiwa na Julius Mawimbi Kisena ‘Mawimbi’ mkazi wa Mazizini Ukonga, Dar karibu na Kituo cha Polisi Mazizini ameonekana kuwa kivutio kwa watu wa eneo hilo kutokana na kufanya vitendo vya kibinadamu. Mapaparazi wetu walimtembelea (Mawimbi) katikati ya wiki hii, nyumbani kwake hapo na kufanikiwa kuongea na ‘bosi’ wake huyo ambaye alikiri mbuzi huyo kuwa na maajabu kibao.
ANAPENDA KULA ‘BATA’ Kwa kawaida mbuzi hujulikana kwa kula majani, lakini ‘Mawimbi’ yeye anapenda kula ‘bata’, vyakula kama nyama choma, nyama iliyopikwa, maandazi, chapati kwa mchuzi, ubwabwa kwa nyama, ugali, chipsi kavu na mihogo ya kukaanga ndiyo mwake. Ili kudhihirisha hilo, Mawimbi aliwaagiza waandishi waliopiga hodi nyumbani kwake kwenda gengeni kununua chapati ili waamini kile anachokisema juu ya mbuzi huyo mwenye uzito wa kilo 128. “Ili muamini kweli mbuzi wangu anakula vyakula vya binadamu, nendeni mkanunue chapati mumletee, mtaona atakavyozifuta chapchapu,” aliagiza Mawimbi. Mapaparazi wetu walikwenda gengeni jirani na makazi ya mbuzi huyo na kununua chapati tano ambapo alipopelekewa, alizifuta
BIA KWA SANA Mawimbi aliongeza kuwa mnyama huyo anakata kilevi kama hana akili nzuri. Alisema amekuwa akinywa aina zote za bia na ana uwezo wa kunywa za baridi zaidi ya 18 kutokana na uhitaji wake kwa siku bila kupepesuka wala kuwa bwii. Je, Mawimbi anajuaje kama mbuzi wake ana kiu ya bia? “Mara nyingi akipata hamu ya bia huenda kwenye baa na kuzungukazunguka hapo mpaka atakapohudumiwa. “Kama akiwakuta watu wanakunywa huwasogelea na kuwaangalia kwa macho yenye uhitaji. Wanaomfahamu humnunulia na kumwekea kwenye chombo na kumpa. Wasipotekeleza hilo hufanya fujo kwa kupiga kichwa meza za wateja mpaka kuangusha vinywaji vyao,” alisema Mawimbi. LAKINI MBAKAJI! Kila kizuri kina kasoro, wakati mbuzi huyo analeta mshangao kutokana na tabia yake hiyo lakini kumbe ana tabia za kubaka wanawake, hasa wale walio kwenye siku zao. “Tatizo la mbuzi huyu ana tabia ya kubaka wanawake, hasa wale walioko kwenye siku zao,” alisema Mawimbi. Akaendelea: “Amini usiamini hadi sasa ana kesi 18 za kubaka katika Kituo cha Polisi cha Mazizini. Waathirika wakubwa ni wanawake hao ambao hupita karibu yake. “Yeye akishasikia harufu ya mwanamke tu huanza kumkimbiza kwa lengo la kupata mambo ya kiutu uzima.” AKIIBWA ANAKUWA MZITO KULIKO TEMBO! Hili nalo, Mawimbi analisimulia kama maajabu mengine ya mbuzi wake, kwamba alishawahi kuibwa mara 3 bila mafanikio kwani wezi hao walimrudisha wenyewe baada ya kuelemewa
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

2 comments:

  1. Huyo mbuzi atakuwa wa kishirikina haiwezekan kabisa mungu akampa tabia za ajabu hivyo......

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wa kishirikina huyo hana lolote ,, na huyo mmiliki wake atakuwa chawiii tuu

      Delete

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs