Chaguzi baada ya chaguzi, ipo mikoa tunaona jinsi inavyotamalaki ushindi wa CDM kila chaguzi zinapofanyika, na zile ambazo zina bank kura nzuri pamoja na kwamba tunashindwa na zile ambazo zinaonyesha kudorora kwenye kila chaguzi.

Chama hiki cha siasa ni chama kinachokuwa kwa kasi kina hitaji viongozi makini, wasomi, na wenye uwezo mkubwa wa kuona mambo, kupambanua na kutenda. Natumaini viongozi wetu wa chama wa mikoa na wilaya, tarafa na kata ni wale wenye weledi wa kuthubutu na kufikia viwango halisi vya viongozi.

Uongozi unaonekana kwa kiwango cha kuweza kufikia malengo uliyopewa, kiongozi wa kisiasa wa mkoa na wilaya ndio wana hakikisha ukuzi wa chama ngazi husika wakishirikiana na viongozi wa kata na vijiji. Kuna haja ya kufanya tathimini kama hawa viongozi wana fanya kazi zao ipasavyo. haiwezekani wilaya nzima tukakosa hata kata moja kwa Udiwani au mkoa mzima tukakosa ubunge.

Viongozi wanaotegemea mpaka viongozi wa taifa wafike ndio wafanye kazi hawatufai. lazima chama kijikite na kujijenga ngazi ya kata, wilaya na mkoa ili kuweza kuwafikia wengi kwa wakati muafaka.

Chaguzi zinatoa mwanga wa kukua kwa chama kwani kura zinaonyesha chama kinakuwa, sasa umakini unahitajika zaidi kuliko wakati wowote. Hakuna wa kulaumiwa 2015.

Imeandikwa na Chief Mkwawa wa kalenga
Hatukumshinda mkoloni kwa imani, bali kwa vitendo.