WAZIRI MKUU WA ZAMANI, BERLUSCONI WA ITALIA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 4 JELA.

Silvio Berlusconi.
Mahakama moja mjini Milan imemhukumu Waziri Mkuu wa zamani wa Italia Silvio Berlusconi kifungo cha miaka minne gerezani kwa kukwepa kulipa kodi na kumpiga marufuku kushikilia wadhifa wa umma kwa miaka mitatu.
Uamuzi huo wa mahakama umekuja siku mbili baada ya mfanyabiashara huyo na mwanasiasa mwenye umri wa miaka 76, kutangaza kuwa hatagombea tena nafasi ya Waziri Mkuu katika uchaguzi wa mwaka ujao.
Mwendesha mashitaka Fabio De Pasquale amehoji kuwa kampuni ya habari ya Berlusconi, Mediaset, ilikuwa na mfumo wa kifedha wa kuongeza kiholela malipo ya haki miliki za televisheni kutoka Marekani kwa njia ya kampuni zilizosajili nje ya nchi.
Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka kampuni ya Berlusconi ilikwepa Klipaji kodi yenye thamani ya Euro bilioni 14 kwa miaka kadhaa.
Mo Blog
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs