CHADEMA KUWA GUMZO KATIKA MKUTANO WA CCM INAMAANISHA KUWA NI CHAMA IMARA

KIVULI cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kinaonekana kukitisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya jina la chama hicho kutawala katika mkutano mkuu wa CCM uliomalizika Jumanne mjini Dodoma.
Jina la Chadema lilianza kutawala katika mkutano 
huo, Jumapili Novemba 11 mwaka huu,  wakati makada wa chama hicho 
waliokuwa wakigombea ujumbe wa Halmashauri Kuu (Nec), wakijinadi kwa 
wajumbe.
Chadema ilitumiwa na baadhi ya wagombea wa nafasi 10 za Bara na Visiwani kama kete yao ya kuchaguliwa kupata nafasi hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na 
Uratibu), Stephen Wassira wakati akiomba kura aliwaambia wajumbe wa 
mkutano huo wampe kura ili apeleke kilio Chadema. Alisema akichaguliwa mjumbe wa Nec atapata nguvu ya kupambana na Chadema.
“Nipeni kura ili nipate nafasi nipeleke kilio 
Chadema,” alisema Wassira huku akishangiliwa wakati akiomba kura na Rais
 Jakaya Kikwete akimwita kwa jina la utani ‘Tyson’. Katibu Mkuu wa 
Umoja wa Vijana wa chama hicho, (UVCCM), Martine Shigela  wakati akiomba
 kura kwa wajumbe wa mkutano huo alisema yeye ndiye anayeongoza jeshi la
 ardhini  linalopambana na wapinzani wanaopiga kelele.
“Mimi ndiye ninayeongoza jeshi la ardhini linalopambana na wapinzani wanaopiga kelele,” alisema.
Naye Mwanamanga Manguga aliwaomba wajumbe wampigie
 kura ili CCM aipeleke Chuo Kikuu cha Dodoma anakosoma na kwamba, tayari
 ameshaingia katika mapambano.
Alisema katika uchaguzi wa udiwani uliopita Kata ya Msalato mjini Dodoma, wafuasi wa Chadema walimpiga mawe na kumjeruhi wakati akitetea chama hicho.
Alisema katika uchaguzi wa udiwani uliopita Kata ya Msalato mjini Dodoma, wafuasi wa Chadema walimpiga mawe na kumjeruhi wakati akitetea chama hicho.
Chadema pia ilikuwa ikitamkwa sana na 
mshereheshaji wa mkutano huo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho
 Nape Nnauye wakati akitoa matangazo mbalimbali kwa wajumbe. 
“Watawezaaa… Wataweza hao Chadema…,” alisikika akiwaambia wajumbe wa 
mkutano huo nao wakimjibu; “Hawaweziii!”
Vilevile, Chadema ilikuwa ikitajwa sana na wapambe
 wa wagombea wa nafasi ya Nec ambao mara kwa mara walisikika wakiwaambia
 wachague wagombea wao kwa sababu ndio wenye uwezo wa kupambana na 
Chadema.
Mpambe mmoja wa mgombea mmoja ambaye hakupenda 
kutajwa jina lake, aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa chama hicho 
kinapaswa kuchagua safu ya uongozi ambayo itakuwa ni mwiba kwa Chadema.
Hata Rais Jakaya Kikwete wakati akifunga mkutano 
huo, Novemba 13 mwaka huu, aliwataka wanachama wa chama hicho kuwajibu 
wapinzani kwa hoja, kama alivyofanya, aliyekuwa Katibu wa Uchumi na 
Fedha wa chama hicho, Mwigulu Nchemba wakati wa Bunge la Bajeti mwaka 
huu.
Alisema, “Baada ya wapinzani kutoa bajeti yao, 
kijana wetu, Mwigulu alisimama akaivunjavunja bajeti yao. Wakanywea.  
Ndivyo tunavyopaswa kufanya.
 
 
 
 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII