KATIKA PICHA: OBAMA AKIREJEA WHITE HOUSE BAADA YA USHINDI....TAZAMA PICHA ZAIDI HAPA

Obama na familia yake wakirejea Ikulu ya Marekani.
Familia ya Kwanza (First Family) ya Marekani, Obama, binti zake, Malia na Sasha, na mkewe Michelle, ikiingia Ikulu katika njia iliyotengenezwa maalum.
Obama na familia yake wakishuka kwenye ndege tayari kuelekea Ikulu.
Ikulu ilivyokuwa inang’aa kuikaribisha familia ya Rais Obama.
Wakienda kupanda gari la kuwapeleka uwanja wa ndege Chicago.
“Baibai!” wanasema Obama na mkewe wakiwa tayari kupanda ndege.
Mgombea mwenza  Joe Biden na mkewe, Jill, wakiwa tayari kupanda ndege ya Air Force Two baada ya ushindi.
RAIS Barack Obama aliungana na mkewe, Michelle, na binti zake Sasha na Malia, kurejea ikulu huko Washington DC muda mfupi tu baada ya kutoa hotuba ya ushindi wake ambapo amesisitiza kwamba “mambo mema zaidi bado yanakuja”.
Aliongeza kwamba: “Amesikiliza na  kujifunza mengi kutoka kwa Wamarekani wakati wa kampeni .”
(PICHA KWA HISANI YA : AP, AFP/GETTY IMAGES NA REUTERS)
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Copyright © 2013. ArtAfropixels Media.com - All Rights Reserved
Customized by: IT XPERTTZ ONE | Powered by: BS
Designed by: Tilabs