MBUNGE WA ZAMANI WA CCM AJIUNGA NA CHADEMA ....SOMA ZAID HAPA
Mbunge wa zamani CCM katika majimbo ya Mpwapwa na Kongwa Gideon Senyagwa
amekihama chama hicho na kujiunga na chama cha CHADEMA.Mbunge huyo
alipewa kadi Na. AO CDM 0101716.
Mbunge huyo wa zamani alihamia CDM Novemba 9 pamoja na makada wengine wa CCM wakiwemo Mkiti wa Tawi la Ngh'umbi Boazi Madukani na Katibu wa Tawi hilo Mbagilwa Festo.Pia CHADEMA imezoa wanachama 260 katika jimbo hilo kama ishara ya kuunga mkono uamuzi wa mbunge huyo wa zamani.
Akihutubia maelfu ya watu katika mkutano uliofanyika Kibaigwa Senyagwa alisema kuwa hafurahishwi na vitendo vinavyofanywa na CCM ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa mmomonyoko wa maadili kutoka kwa baadhi ya viongozi huku wakipuuza kero za wananchi.
Aliwataka wananchi kote nchini kuunganisha nguvu na CHADEMA kuiondoa CCM madarakani.Amesema CCM inapaswa kujua mwisho wake umekaribia kama hata mtu kama yeye ameamua kukiacha chama hicho.
Source: Tanzania Daima.

0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII