MISS EAST AFRICA 2012 KUFANYIKA TAREHE 7 DESEMBA MLIMANI CITY DAR ES SALAAM
Mrembo atakayeiwakilisha Somalia katika mashindano ya Miss East Africa mwaka huu ametangazwa rasmi.
Mrembo huyo mwenye urefu wa futi 5.9 anaitwa HALIFA AYAN YUSUF aliyezaliwa Somalia Hargeisa na ana umri wa miaka 21.
Fainali za mashindano ya Miss East Africa
2012 zitafanjika tarehe 07 mwezi Desemba mwaka huu katika ukumbi wa
Mlimani City jijini Dar es salaam ambapo zitashirikisha Nchi za
Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea,
Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na
Mauritius.
Mashindano ya Mwaka huu yanayosubiliwa kwa
hamu yanatarajiwa kushuhudiwa na mamilioni ya watu Duniani kupitia
kwenye luninga zao na pia kwa njia ya Internet ambapo yatautangaza
utalii wa Tanzania kwa kiasi kikubwa na pia kujenga umoja wa Afrika
mashariki na kudumisha utamaduni wa ukanda huu wa Afrika.
Mashindano ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltdya jijini Dar es salaam.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII