PICHA ZA YANAYOJIRI KWENYE NDEGE INAYOMZUNGUSHA RIHANNA KWENYE TOUR 777......INGIA HAPA

Rihanna akiwa na marubani wa ndege ya tour yake
Wakati ndege ikiwa angani mashabiki wa Rihanna waliopata bahati ya kualikwa kwenye tour hiyo pamoja na waandishi wa habari wapatao 150 kinachooendelea ni kula bata na mtungi kwa kwenda mbele.
Katika wakati mmoja safari hiyo iliingia dosari kidogo baada ya mwandishi mmoja kuamua kuvua nguo zake wakati ndege ikiwa hewani na kuamsha kelele na shangwe nyingi kwenye ndege hiyo.
Safari hiyo imeingiwa na dosari baada ya Rihanna kukataa kufanya interview na mwandishi yeyote na kumfanya mtangazaji huyo wa Fox FM ya mjini Melbourne, Australia kuvua nguo zake.
Wengine wanalalamika kuwa Rihanna amekuwa akitumia muda mwingi amejifungia kwenye chumba cha dharura.Pia huduma ya chakuka kwenye ndege hiyo imekuwa ikilalamikiwa na watu hao wanaodai kulishwa vyakula vya ajabu ajabu.
Wengine wanadai kuwa hawana muda wa kupumzika licha kufikia kwenye hoteli za kifahari ambako hulala kwa saa mbili au tatu tu kabla ya kuamshwa tena kuanza safari ya nchi nyingine.
Leo Rihanna atakuwa na show jijini London na tayari ameshaperfom Mexico City, Toronto, Stockhom, Berlin na Paris.
Hizi ni baadhi ya picha za ndani ya ndege hiyo na zile anazotumbuiza kwenye ziara hiyo.
- Rihanna akiwa na marubani wa ndege ya tour yake
- Rihanna akiwa na furaha ndani ya ndege kama vile ametoka kuongea na Chris Brown kwenye simu
- The beautiful Rihanna
- Rihanna kwenye stage
- Akiwa uwanja wa ndege baada ya kuwasili
- Rihanna, mashabiki wake na waandishi wa habari wakifurahia safari
- Take as many photos as you can!!
- Rihanna akiperform mjini Stockhom Sweden
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII