Leo ndo yalikuwa ni mazishi ya Padri Evaristus Mushi aliyepigwa risasi akiwa katika utekelezaji wa majukumu yake na hivi sasa ndo kuaga na kufanya misa ya marehemu. Watu wengi mno na viongozi wa serikali,siasa na dini ya kikristo wamehudhuria. Baadhi ni rais wa zanzibar Dr. Shein, Dr. Slaa,mchungaji Mtikila. Walipotakiwa kueleza wameguswa vipi na kifo cha padri.

Dr slaa amesema ni tukio la kusikitisha kutokea zanzibar kwani znz ndo chimbuko la ukristo kwa Tz. Wamisionari wa kwanza walianzia znz. Ameshangaa haya matukio yanajitokeza siku hizi. Tukio hili halina maelezo ya kina kuhusu chanzo chake. Amesisitiza kuwa tusingependa kifo cha aina hii kitokee kwa mtu yeyote na akasema muda umefika sasa tujadili mizizi ya tatizo na si matawi na matunda ya tatizo.

Naye Mchungaji Mtikila amesema ni muda wa kutafakari,kuonyesha uvumilivu kwa watanzania wote bara na visiwani. Amesema ni kipindi cha kutafakari vitabu vitakatifu vinasema nini. Kwa waislam,amesema korani inasema adui wao si wakristo bali ni mayahudi na makafiri.
Source: Radio Maria