MISS TANZANIA ANASWA NA MUME WA MTU: FATILIA STORY HII HAPA


Chanzo chaanika
Awali, chanzo chetu kilichoomba hifadhi ya jina lake kilidai kuwa, Abed ana mke wake aitwaye Nasra lakini baada ya kukutana na Lisa ‘amekufa na kuoza’ kwake hivyo kujikuta akiwekeza penzi lake.

“Tuliona picha Lisa na Abed wakiwa wote China kwenye mashindano ya Miss World, tukahisi ni kampani ya kawaida tu lakini tumeshangaa kusikia ni wapenzi, kwa kweli inasikitisha.”
Mwandishi wetu alimuomba ‘sosi’ huyo amuibue Nasra ambaye inadaiwa kwa sasa anaishi Uingereza ili afungukie sakata hilo lakini inavyoonekana mwanamke huyo anaogopa magazeti kama ukoma.

Abed asakwa
Baada ya kupata madai hayo, waandishi wetu walianza kumsaka Abed kupitia simu yake ya mkononi ambapo siku ya kwanza hakupokea na hata alipotumiwa meseji na kutakiwa kupokea simu ili asomewe madai hayo, hakujibu chochote licha ya sms kuonesha ‘delivered’.
Siku ya pili alipopigiwa tena hakupokea lakini siku ya tatu (Ijumaa iliyopita) majira ya saa 7 mchana, mwandishi alikuta ‘missed call’ ya Abed na alipopigiwa na kutakiwa kufungukia madai hayo alisema, yeye si mpenzi wa Lisa na kama kuna picha zinazowaonesha wako pamoja, hiyo haimaanishi wanatoka.

Katika hali ya kushangaza, kabla Abed hajamaliza kuzungumza, Lisa ambaye pia ni Miss Tanzania namba 3, 2006 alimpokonya simu (inaonekana walikuwa pamoja) na kufichua siri nzito.
Lisa alisema, anachojua yeye Abed ni mchumba wake na si mume wa mtu licha ya kwamba huko nyuma anajua alishawahi kuwa na wanawake wengine.
“Abed ni mchumba wangu na ukweli ni kwamba mimi nafahamika kwao na yeye anafahamika kwetu kwa hiyo si jambo la siri, ndiyo maana nashangaa hayo madai kuwa eti ni mume wa mtu,” alisema Lisa, maelezo yanayoibua hisia tofauti kufuatia awali Abed kukana kutokuwa na uhusiano naye.

Lisa amekuwa ni staa asiyekuwa na skendo nyingi tofauti na wenzake ambao walifanikiwa kuchukua nafasi za juu kwenye mashindano ya Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, Jokate Mwegelo na Aunt Ezekiel.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII