MMH!! SERIKALI YA KIKWETE YAONGOZA KWA KUKOPA: DENI LA TAIFA LAFIKIA TRILIONI 21
YAKOPA MARA MBILI ZAIDI YA ZILIVYOKOPA AWAMU YA TATU ZILIZOPITA.
http://www.mwananchi.co.tz Febr 23/ 2013.
Kwa ufupi:
Rais Kikwete aliingia madarakani mwaka 2005, baada
ya rais aliye mtangulia, Benjamin Mkapa kumaliza kipindi chake cha
uongozi wa miaka 10 kilichoanzia mwaka 1995 hadi mwaka 2005.Rais wa awamu ya nne Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na vyombo vya habari siku za hivi karibuni
TAASISI isiyo ya kiserikali ina yojishughulisha na masuala ya
Madeni ya Taifa na Maendeleo (TCDD), imesema Serikali ya Tanzania ndiyo
inaongoza kwa kukopa zaidi, ikieleza kuwa kati ya mwaka 2008 hadi mwaka
2011, imekopa kiasi cha Sh15trilioni na kufanya deni la taifa kufikia
Sh21trilioni.
Rais Kikwete aliingia madarakani mwaka 2005, baada
ya rais aliye mtangulia, Benjamin Mkapa kumaliza kipindi chake cha
uongozi wa miaka 10 kilichoanzia mwaka 1995 hadi mwaka 2005.
TCDD imebainisha kuwa Serikali inakopa fedha hizo
kutoka Benki Kuu (BoT), Benki za Biashara, Kampuni za Bima na Mashirika
ya Hifadhi za Jamii. Pia inakopa katika taasisi za kimataifa ikiwamo,
Benki ya Dunia (WB), Benki ya Maendeleo Afrika (ADB) na Shirika la Fedha
Duniani (IMF).
Katika maelezo yake, Mkurugenzi Mtendaji wa
taasisi hiyo Hebron Mwakagenda, alisema kuwa kite ndo cha Serikali
kukopa fedha kwa ajili ya matumizi yasiyo muhimu pamoja na kuwalipa
watumishi wake mishahara, ndiyo sababu ya kukua kwa deni hilo la taifa.
“Serikali ya awamu ya nne imekopa kwa kiwango
kikubwa, kwani tangu iingie madarakani imeshakopa Sh15trilioni, sasa
sijui mpaka inamaliza muda wake itakuwa imekopa kiasi gani?” alisema
Mwakagenda akihoji na kuongeza;
“Hata kama kukopa ni kuzuri basi tukope na fedha
tuzifanyie mambo ya maana hasa katika maendeleo, tukope tu pale
inapokuwa lazima kufanya hivyo.”
TCDD imeeleza kwamba hali hiyo ni hatari, hasa
ikizingatiwa kuwa miaka kadhaa iliyopita, Tanzania kupitia Mpango wa
Nchi Maskini zenye Madeni Makubwa (HIPC), ilifutiwa kiasi kikubwa cha
madeni, lakini sasa imeanza kukopa tena na deni kukua kwa kasi.
Taasisi hiyo pia imesema kitendo hicho kimechangia
kuporomoka kwa uchumi wa taifa kunakosababishwa na riba kubwa za mikopo
hiyo, ambapo kulingana na idadi ya Watanzania ukigawanya deni hilo kwa
wote, inaonyesha kuwa kila Mtanzania anadaiwa wastani wa Sh450,000.
Mwakagenda, ambaye taasisi yake inafanya kazi ya
kuishauri Serikali katika suala zima la deni la taifa na maendeleo,
alisema hadi kufikia Oktoba mwaka jana, deni la nje lilikuwa Sh15.9
trilioni.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali (CAG), aliyoitoa bungeni mjini Dodoma mwaka jana,
taifa linapoteza Sh3 trilioni katika ukwepaji wa kodi na ubadhirifu,
huku akishauri kuwa mambo mawili yakifanyiwa kazi deni hilo litapungua
au kumalizika kabisa.
“Deni linakuwa kwa kiasi kikubwa na tunakopa
katika mabenki ya biashara, ambayo riba yake ni kubwa, fedha nyingi
zinazokopwa hutumika kulipa mishahara,” alisema Mwakagenda.
Alifafanua kwamba mwaka 2007 hadi 2008 deni la
taifa lilikuwa Sh6.4 trilioni na kwamba, kuanzia mwaka 2007 hadi 2011
deni hilo limeongezeka hadi Sh21 trilioni.
0 comments:
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII